Waungwana,
Samahani kidogo wakuu zangu, nataka kuinunua mada maanake naona sasa mnakwenda kusiko.. imekuwa taabu kusoma matusi zaidi ya hoja..
Hivi niulize kitu kimoja.. hii sheria imepitishwa kwa sababu ni haki ya wanawake wote au wa wapi?..Je, wanawake wetu wameulizwa au imechukuliwa tu ni haki kwa sababu nchi za magharibni wamesema hivyo pasipo sisi kuangalia WATU na MAZINGIRA yetu..
Wakuu zangu ni muhimu sana tukumbuke kwamba hata sisi (WATU) pamoja na umaskini wetu tuna mila, tamaduni na desturi zenye miiko na maadili ambayo zinaijenga jumuiya yetu kama Watanzania...Na ni muhimu sana tuelewe hivyo kwanza kabla hajujahukumu kwani kwa kutoelewa mila na desturi za watu, ndio maana tunawalaani wanawake wa kiislaam kuvaa nguo ndefu na hijabu wakati hiyo ni culture ya watu wa Middle East kabla hata ya sheria hiyo kuwa ndani ya Uislaam..isipokuwa dini imesisitiza culture hiyo iendelezwe kwa kuelewa umuhimu wa mila hiyo ktk jumuiya yao. Utakuta mwanamke wa Kitanzania akipinga vazi hilo kwa sababu ambazo hajijengi kwani yeye mwenyewe huvaa khanga na vitenge ku cover area zile zile na akajiona kachomoka..
Hivyo utakuta Wayahudi, wakristu na waislaam waishio nchi hizo kuvaa nguo hizo hata kama sheria hiyo isingekuwepo. Nini hofu ya serikali ya nchi za kiarabu na hasa kuondoka kwa mila hiyo ni kwamba unaporuhusu kuondoka kwa sheria kama hiyo ua kijadi unakaribisha culture nyingine. Ni lazima kuna reprecement, na mara zote hutazamwa faida ya mila inayokaribishwa kutengua mbovu, lakini sii busara kuondosha mila kwa sababu tu nchi za magharibi zinafanya hivyo hali athari zake ni kubwa na mbaya kuliko ile ya asili.
Hivyo nirudi kwenye mada hii, sisi Watanzania swala la utoaji mimba ni haramu toka zamani kabla hata dini hazijafika.. Mume anayemweka mimba binti huadhibiwa kwa huozeshwa kwa nguvu..rape case nadhani ilikuwa ilikuwa kifo hivyo ukitazama utunzi wa sheria zetu pamoja na kwamba hazikuwa nzuri ilikuwa ni KUMLINDA mwanamke..Na mara zote sheria hutungwa KULINDA victims na kuadhibu wale wanaokiuka sheria hizo lakini kuhalalishi maovu hakuwezi kuwalinda wanawake bali kuwaongezea zaidi matatizo yanapohalalishwa..
Unapohalalisha Uotaji mimba ni ni sawa na kuwaambia wanaume (sii wanawake) kuwa mchezo wa kutia mimba wasichana wadogo, ku rape wanawake na kadhlika ni halali kwani ufumbuzi wa uovu huu unatolewa hoispital. Na ushahidi unaonyesha wazi kwamba nchi zote zinazoruhusu utoaji mimba zina ongezeko kubwa la uotaji mimba kila mwaka kuliko nchi zinazopinga sheria. Rape case na uasherati huongezeka lakini ni case chache sana hufikishwa mahakamani kwa sababu ufumbuzi wa hospital huificha siri kubwa..Ni rahisi kwa mwanamke kwenda kutoa mimba hospital akaficha yaliyotokea kuliko kuanika achafu uliotendeka, Hivyo mfumo mzima wa ruksa hii huwafuga wabakaji wakaishi baina yetu bila kuadhibiwa.
Ni muhimu kwetu kutambua kwamba mimba yoyote isiyotakiwa ni mimba iliyopatikana kwa uharamu fulani, hivyo yupo mwanamme mwenye makosa na anatakiwa kufikishwa mbele ya sheria ili kuwalinda wanawake ili kumwondoa mhalifu ktk society.
Kwa hiyo sheria kama hii ni lazima iambatane na vikwazo ambayo vitaifanya sheria hii kuwa almost impossible kwa mhalifu kushiriki au kuendelea na vitendo hivi. Ruksa ya kutoa mimba haipunguzi matatizo yanayotokana na mimba hizo isipokuwa inaongeza tatizo la mimba sizizotakiwa na pia kuondoa kabisa mila na desturi zetu zilizotujenga toka zamani..
Binafsi naamini kabisa kwamba mimba hutungwa kwa matakwa yetu, cases za rape ni chache sana kiasi kwamba hatuwezi kuhalalisha utoaji mimba isipokuwa kwa wale tu walioathirika, na Hospital itatumika kama sehemu ya kuponya (kuondoa mimba) cases ambazo zinakubalika ktk jumuiya yetu...