Serikali ya Tanzania yazuia ndege kutoka shirika la Kenya Airways kutua Dar, Kilimanjaro na Zanzibar

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imefuta kibali cha ndege kutoka shirika la Kenya Airways kutua katika viwanja vya ndege vya Zanzibar, Dar es Salaam na Kilimanjaro kuanzia tarehe 1 Agosti 2020. Maamuzi haya yametolewa kama majibu (reciprocal basis) kutokana na maamuzi yaliyochukuliwa na serikali ya Kenya ya kuzuia ndege kutoka shirika la ATCL (Air Tanzania Company Limited) kuingia nchini Kenya kwa madai ya kuanza kuruhusu nchi zenye maambukizi madogo ya corona.

Maelezo zaidi yametolewa kwenye barua hii iliyoambatanishwa.

 
HAHAHAHA, Kelele za chura hiyo. Uganda ama Rwanda zikifunga Kenya inaweza kuumia lakini si Tanzania. KQ na mtoto wake Jambo Jet zinaenda Entebbe na Kigali kushinda Dar na hizo vitu zingine umetaja
 
Pagumu sana hapa! MKAPA ndio alikuwa anaweza kumshauri Magufuli sasa hayupo[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Yaani diplomasia ya Kenya na Tz ipo pabaya sana.

Ego itaua uhusiano wa hizi nchi mbilii japo wanajidai marafiki kinafiki lakini tushafikaa mbalii aiseee sasa hivi raia wa Tanzania wataanza kutimuliwa Kenya[emoji29][emoji29]

MKAPA majirani wote hawajaja kumzika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…