Serikali ya Tanzania yazuia ndege kutoka shirika la Kenya Airways kutua Dar, Kilimanjaro na Zanzibar

Kwa hiyo wamezuia precision na si watanzania siyo? Huo Mambo ya uchumi yanahusu nauli anazokusanya precision au interaction ya watu wa nchi hizo mbili? Kwamba wakibebwa na KQ iwe uhujumu uchumi
 
Kwamba watanzania hawaruhusiwi kupanda KQ au sijakuelewa?
 
Hi nchi inaharibiwa Kwenye anga za mahusiano ya kimataifa na mgonjwa wa akili.
 
HAHAHAHA, Kelele za chura hiyo. Uganda ama Rwanda zikifunga Kenya inaweza kuumia lakini si Tanzania. KQ na mtoto wake Jambo Jet zinaenda Entebbe na Kigali kushinda Dar na hizo vitu zingine umetaja
Unajifariji na ni vizuri kufanya hivyo. Hizo KQ hufanya safari Tz zikileta hata watalii kutoka Ulaya na Marekani. Itabidi watafute mashirika mengine ya kuwaleta Tz, KQ wataendelea kupata hasara.

Vv
 
Kwa hiyo wamezuia precision na si watanzania siyo? Huo Mambo ya uchumi yanahusu nauli anazokusanya precision au interaction ya watu wa nchi hizo mbili? Kwamba wakibebwa na KQ iwe uhujumu uchumi
Uwelewe mahusiano Kati ya nchi na nchi lazima kuwe na usawa hata kama hupati faida hiyo ndio kanuni duniani kote .mfano Kenya ina balozi TANZANIA na TANZANIA ina balozi Kenya endapo TANZANIA itafunga ubalozi wa Kenya na Kenya itafunga tu hata kama itakua wakenya wanafaidika Watanzania kwenda kwao bado wataufunga tu lazima kuwe na usawa unaposema Uganda inaruhusiwa halafu Tanzania hairuhusiwi wakati hizo nchi zina share mipaka ,Ziwa victory huoni tatizo hilo mkuu? du!!
 
Mkuu rikiboy jitahidi uondokane na mawazo ya uoga. Nchi ni lazima ilinde heshima yake.
 
Mkuu huo usawa unaousema hapa ni upi? Ndege zetu kwenda Kenya au watanzania kuwa na Uhuru wa kwenda Kenya na wakenya kuwa na Uhuru wa kuja bongo? Kama ni ndege zetu kwenda je hapo kabla ndege gani za Tanzania zilikuwa zinaenda Kenya na zilikuwa na flight ngapi ukilinganisha na KQ? Ninaposisitiza tuache mihemuko najua ninachoongea
 
Mkuu naona unaendeleza akili zile zile za kuiombea matatizo nchi yako mwenyewe.

Lazima heshima ya nchi ilindwe, huu sio muda wa kupigia magoti binadamu dhaifu kama wewe.
 
Ww unafikir chakula wanatoa mbinguni?
Tz ndo ina ardhi kubwa ya kusupply chakula na kuna magari mengi ya kutoka kenya kuja kubeba msosi huku. Pia msoc ni bei rahisi kuliko sehemu nyingi za Africa na duniani na ni rahisi kuupata but bidhaa zitokazo kenya ni rahisi kupatikana kwengine nje ya kenya so wao hawana umuhimu kwetu
 
Mkuu naona unaendeleza akili zile zile za kuiombea matatizo nchi yako mwenyewe.

Lazima heshima ya nchi ilindwe, huu sio muda wa kupigia magoti binadamu dhaifu kama wewe.
Heshima ya nchi haijawahi kulindwa kwa maamuzi ya kukurupuka na mihemuko,sana sana tutaonekana watu wa ajabu
 
Oh yeah?

You my brother,are a fool!
 
MUTUA: Tanzania ni jirani jeuri, tuvumilie kuishi naye

Na DOUGLAS MUTUA
NCHI inapojipata na jirani mbaya ilhali yenyewe haiwezi kuhama au kumhamisha, inapaswa kufanya nini?
Nimeandika hapa kwa takriban miaka mitano sasa, tangu Dkt John Pombe Magufuli achaguliwe rais Tanzania, kwamba taifa hilo si rafiki bali adui.
Japo halijatangaza uadui wa wazi, kuna mifano kadhaa ya mambo ambayo ukijumuisha moja na moja, utapata hesabu kamili: Tanzania si rafiki wa Kenya.
Juzi tu, ujumbe wa waombolezaji kutoka Kenya uliokuwa njiani kuelekea Tanzania kuhudhuria ibada ya wafu ulirudishwa nchini katika hali isiyoeleweka vyema.
Nimesema hali isiyoeleweka vyema kwa sababu waelekezi wa safari za ndege nchini Tanzania walisema hali mbaya ya hewa haingeruhusu ndege hiyo ya Kenya kutua.
Ujumbe huo ulikusudia kumwakilisha Rais Uhuru Kenyatta katika ibada ya kumuaga aliyekuwa rais wa tatu wa Tanzania, Bw Benjamin Mkapa.
Uliongozwa na kiongozi wa wengi kwenye Bunge la Seneti, Bw Samuel Poghisio, na ulisafiri kwa mojawapo ya ndege maalumu zinatotumiwa na rais wa Kenya na watu mashuhuri. Ndege hiyo, ambayo tayari ilikuwa imevuka mpaka na kuingia Tanzania, ilinyimwa ruhusa ya kutua hivyo ikabidi irejee ilikotoka.
Katika juhudi za labda kuficha uzito wa tukio hilo, Bw Poghisio alidai ujumbe wake uliagizwa ama urejea Kenya au usubiri hewani kwa muda.
Na kwa sababu kwenye Bunge la Seneti kulipangiwa kuwa na majadiliano muhimu kuhusu ugavi wa pesa za ugatuzi, alidai Bw Poghisio, alilazimika kurejea Kenya.
Wataalamu wa masuala ya kiutawala na kidiplomasia watakwambia hakuna shughuli muhimu nchini kokote kuliko kumwakilisha kiongozi wa nchi kwenye hafla ya kimataifa.
Kikawaida, mjumbe aliyetumwa na kiongozi wa nchi hufanya kila juhudi kuhakikisha ametekeleza wajibu wake. Kisa na maana ni kwamba anaiwakilisha nchi.
Kwa kifupi tu, tunaweza kusema Tanzania iliizuia Kenya kuhudhuria ibada ya wafu ya rais wake wa tatu, Mzee Mkapa.
Hebu niseme moja kwa moja kwamba, binafsi nalitilia shaka dai hilo la hali ya hewa kuwa mbaya. Safari hiyo haikuwa ya kushtukiza; hali ya hewa inatabiriwa hata wiki mbili kabla.
Vile vile, kuna njia kadhaa za ndege kupitia ili kutua kwenye uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Katika ulimwengu wa kidiplomasia, nchi ikitaka kuidharau nyingine, huwatuma wawakilishi wa ngazi ya chini kwenye hafla za nchi inayolengwa.
Nchi hiyo nayo ikishuku tu kwamba hizo ni dharau, hukazana kuidhalilisha iliyozuka na dharau, hivyo hali ikawa ya vita baridi.
Nashuku kwamba kwa upande wa Kenya, hili ni suala la tahadhari tu kuhusiana na janga la Corona, hasa ikizingatiwa kwamba Tanzania na jeuri yake imesema hakuna Corona.
Kumbuka Kenya ilipofunga mpaka wake na Tanzania, taifa hilo la Magufuli liliteta vikali na kuzuia yeyote au chochote kutoka Kenya mpaka Rais Kenyatta akalazimika kuingilia kati.
Haikosi Kenya ililazimika kumtuma Bw Poghisio na ujumbe wa watu wawili pekee badala ya Rais Uhuru Kenyatta kuhudhuria ibada hiyo na kuhatarisha maisha yake.
Hapa unatambua kuwa kuhusiana na jirani mkorofi, ni lazima uwe mwangalifu sana. Katika kisa hicho cha juzi, Kenya ilikabiliwa na hatari mbili za kumkasirisha jirani huyo: siasa za corona na maadili ya kidiplomasia.
Hatua ya pekee ambayo ingekubalika machoni pa Tanzania na Rais Magufuli ni Rais Kenyatta mwenyewe ahudhurie ibada hiyo au amtume Naibu wake, Dkt William Ruto.
Tukubaliane kwamba shughuli muhimu za nchi haziwezi kuwa kuifurahisha nchi nyingine, ndiposa naiunga mkono hatua ya Rais Kenyatta kutofika.
Hata hatua ya kutuma ujumbe Tanzania haikufaa kitu; hakuna maisha ya Mkenya ambayo yanapaswa kuhatarishwa ili tuifurahishe nchi nyingine. Tuna jirani mbaya, hebu tubuni mikakati ya kumdhibiti.

NB: TANZANIA NA WATANZANIA NI LAZIMA KUENDELEA KUWA IMARA KWA MUSTAKHABARI WA NCHI KAMA WENZETU WANAVYOSIMAMA NA NCHI ZAO.
 
Kwamba watanzania hawaruhusiwi kupanda KQ au sijakuelewa?
Kwani unaelewa sababu ya kutangazwa hizo nchi 11 au hauelewi maana ckuelewi hata nn unachomaanisha unaonekana kama mada huijui. Sasa Watanzania kupanda Kq ndio itakua suluhisho la kutokua na korona TANZANIA ? Ndio maana unaambiwa Kenya wanajaribu kutumia korona kuhujumu uchumi wanavutia kwao
 
Mkuu naona unaendeleza akili zile zile za kuiombea matatizo nchi yako mwenyewe.

Lazima heshima ya nchi ilindwe, huu sio muda wa kupigia magoti binadamu dhaifu kama wewe.
Nchi sio CCM mzee

Nchi sio bwana mawe

Nchi sio Abbas

Nchi sio Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja..

Nchi ni wananchi Watanzani who are loving hardworking people!

Hao niliowataja ni watu binafsi wenye akili binafsi zenye kufanya mambo ya hovyo kama mimi na wewe!

Wameona tatizo,badala ya kutatua kwa kutumia akili,wamefanya maamuzi ya chooni

Lazima tuwaseme na tu-demand answers from them,tumewapa ajira na tunawalipa!

We didnt employ them for this nonsense they are doing!

Acheni mihemko ya kipumbavu ya huko machakani Chattle,tunataka sober minds zenye kujua kucheza this economic chess!

Kaanza Kenya,watafata wengine kupiga ban,you dont have answers to all these coming tragedies!

Tunataka jawabu la kwanini wanatudanganya na korona,kwa evidences...hawana wanatuletea stori za Abbas and his minions eti "TZ hakuna corona" sababu madomo yao yanaweza funguka kutamka kitu....evidence?hakuna

Subiri anafuata SA,anakuja UG,then Rwanda,Ulaya na America ndio sahau kabisa....wait and see!
 
Kila mtu ashinde mechi zake
 
Mkuu naomba uiniekeweshe,je waliozuiwa kwenda Kenya ni watanzania au ni ndege za Tanzania?maana ninachojua Mimi wakenya wametangaza ndege za nchi 11 zinazoruhusiwa kutua kwenye viwanja vyao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…