Tetesi: Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK-JMT) yanukia Tanzania Bara

Kuutoa unaibu Uwaziri mkuu kwa lengo la kupima utendaji sioni tatizo, hasa baada ya nafasi hiyo kuthibitishwa rasmi kisheria na kikatiba, ccm haiwezi kugawa nchi ki hovyo hovyo, unaweza kugawa nchi kwa wasio stahili ukatengeneza balaa la ajabu, Nchi sio Shati ujaribu jaribu.
 
Hizi serikali za umoja wa kitaifa ni mbinu ya vyama vinavyog'ang'ania kubaki madarakani kuwapumbaza wenye haki ya kukaa madarakani. Na mbinu hii huwasaidia zaidi chama tawala na sio wapinzani. CDM wakikubali huu utapeli nitawatoa maanani.
 
Umesahau kuhusu Lowassa mlisemaje?
🤣🤣🤣🤣🤣

Ukisoma comments za hao jamaa zetu unaishia kucheka tu na kuamua kunyamaza maana ni kama wana matatizo fulani hiviiii......

Siachi kumpa heshima zangu huyu mwamba, Mbowe, jamaa sayansi ya kufubaza anaijua hwaswaa.............apewe maua yake!!!
 
Kumbe kelele zooote za wanasiasa ni kwa ajili ya kupata vijinafasi vya vyeo huko Jikoni ???!!!
Aasalaaaleeh wananchi bado tutaisoma namba Kwakweli 😅😅😅😱
 
Katiba hairuhusu hiyo kitu.
Kwa mujibu wa Katiba, chama chenye wabunge wengi ndicho kitatoa Waziri mkuu.
Na Waziri mkuu atatokana na mbunge wa kuchaguliwa jimboni.
Kwa bunge la sasa chama chenye wabunge wengi ni CCM.
Naelewa vyema hilo, rudi kasome upya nilicho quote upate connection Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…