Serikali ya Zimbabwe yaipa Leseni Starlink kutoa huduma za Intaneti

Serikali ya Zimbabwe yaipa Leseni Starlink kutoa huduma za Intaneti

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1716665385829.png

Mamlaka ya Udhibiti wa Posta na Mawasiliano (POTRAZ) imeidhinisha leseni ya utoaji Huduma za Intaneti kwa kampuni ya #Starlink inayomilikiwa na Bilionea #ElonMusk

Taarifa ya Rais Emmerson Mnangagwa imesema "Uamuzi huu unatarajiwa kuongeza miundombinu ya Mtandao wenye Kasi ya Juu na ya gharama nafuu kote nchini na hasa katika maeneo yote ya vijijini,"

Uidhinishaji wa Starlink umekuja baada ya kuwepo msako mkali nchini humo dhidi ya Watumiaji wa huduma hizo ambao hawajasajiliwa na wanaouza vifaa vya Starlink kinyume na Sheria

Hadi sasa, Starlink imepata Leseni za huduma katika Nchi za Nigeria, Msumbiji, Zambia, Kenya, na Malawi. Aidha, hivi karibuni nchi za Tanzania na Cameroon zilikamata waingizaji wa Vifaa hivyo wasiokuwa na Vibali.

===========

HARARE, May 25 (Reuters) - Zimbabwe's telecom regulator has approved the licensing of Elon Musk's Starlink, allowing the satellite unit of SpaceX to operate in the southern African country, President Emmerson Mnangagwa said on Saturday.

The decision "is expected to result in the deployment of high speed, low cost, LEO (low-Earth-orbit) internet infrastructure throughout Zimbabwe and particularly in all the rural areas," Mnangagwa said in a statement.

He said Starlink will provide services through its sole and exclusive local partner, IMC Communications.
A World Bank report in 2021 said only 34.8% of Zimbabwe's population had access to the internet.

The country's internet service is dominated by three major mobile network operators.

The Starlink approval comes amid a government crackdown on unregistered users smuggling Starlink kits from neighbouring countries like Zambia.

Starlink is currently officially offered in various African nations, including Nigeria, Mozambique, Zambia, Kenya, and Malawi.

Last month, Cameroon ordered the seizure of Starlink equipment at the country's ports of entry as the provider was not licensed.
 
Ni swala la muda tu watakubali iingie na hakuna kitu watafanya kuizuia. Star link ni kama tumbo la mchafuko au la kuendesha, likikufikia usihangaike kulizuia bali pambana kutafuta choo haraka utulie ushushe vitu, ukileta ligi imekula kwako.
 
Nape naye anatuangusha. Huyu ni mwekezaji mwenye tija pengine kuliko hata DP WORLD.

Roboti lile kwa mm sioni tija yake ,kheri ata mganga wa kienyeji anaweza kupiga ramri lenyewe ndo lishatafuna pesa na hivyo basi litakuwa linakaaga bungeni au wapi ,na Bado litataka service

Nchi hii Mungu tusaidie
 
Starlink haipo Uganda ila Waganda hawakatazwi kutumia kama unayo hivyo watu wamekua wakizinunua kutoka Kenya kwa fujo.

Starlink haipo South Africa lakini Ukiwa nayo hukatazwi kutumia.

Tanzania juzi wamekatama watu kigamboni wanazo Starlink wamewashtaki.

Mimi kwenye kata yetu, hakuna mtandao wa voice wa kuaminika, sio voda, sio Airtel, sio tigo wala halotel, ni kama haipo. Ukija kwenye internet ndio balaa.

Shule ya sekondari ya hapo kijijini kwetu kuna mfadhili tulipata kutoka Marekani, akatuletea computer na kujenga computer lab lakini hakuna mtandao, watoto hakuna kitu wanajifunza. Hakuna mtandao wowote.

Starlink ingekuja tungenunua tu moja tukaweka pale shuleni watoto wakajifunza bila tatizo.

Nchi zilizoendelea kama Brazil, Malaysia nk wanasaini mikataba na Elon Musk kutoa huduma ya Internet vijijini kwenye mashule watoto wajifunze bila tatizo, Tanzania tunasema Starlink wajenge ofisi.

Juzi hapa Putin alisema, Elon Musk ni mtu wa kushirikiana nae kwenye kuleta maendeleo, huwezi kupambana nae. Sisi sijui tunapambana nae kumkomoa ama tunajikomoa wenyewe.

Bado Tuna safari ndefu sana
 
Mimi nafikiri viongozi wetu wanatumika na kama sio basi wameshahongwa mamilioni ya pesa na mitandao ya simu ambayo kwa ujumla wake ni "majambazi wanyonyaji" waowaibia wananchi katika vifurushi vya data, ambao wanajua siku starlink itakapota kibali nchini basi ndio utakuwa mwisho wao.
 
Hawaitaki Starlink sababu watashindwa ingiza mikodi ya ajabu ajabu
 
Musk ameweka kitu kinaitwa global roaming kwenye starlink, hivyo Tanzania inashika vyema.
Tanzania mbona watu wanatumia wengi tu. Wajanja wanavitumia sana.

Wanaviagiza Kenya, uzuri ukikiweka hata sakafuni kinashika si lazima juu ya bati, kama nyumba ina uzio ukikiweka uwani chini kinashika fresh tu.
 
Mambo yote mazuri yanaenda Zanzibar asa hivi, huku bara yanapita tu.
 
Musk ameweka kitu kinaitwa global roaming kwenye starlink, hivyo Tanzania inashika vyema.
Tanzania mbona watu wanatumia wengi tu. Wajanja wanavitumia sana.

Wanaviagiza Kenya, uzuri ukikiweka hata sakafuni kinashika si lazima juu ya bati, kama nyumba ina uzio ukikiweka uwani chini kinashika fresh tu.
Subscription yake inakuwaje sasa?
 
Nape huwa anakua na akili timamu akiwa hana cheo chochote
 
Back
Top Bottom