Chato ninayoifahamu, ilihitaji sana huduma nyingi zinazogusa wengi, kabla ya uwanja wa ndege.
Sasa ni lazima Serikali irudi kwenye mahitaji ya msingi yanayogusa wananchi walio wengi wa Chato kuliko kukazania vitu vya showoff, visivyo na impact kubwa kwa umma.
Kuna wakati Chato itahitaji sana uwanja wa ndege, lakini wakati huo siyo sasa. Kuwajengea VETA ilikuwa sahihi, kuwajengea hospitali nzuri ya kawaida yenye vifaa na huduma zote muhimu, ilikuwa sahihi, lakini hospitali teule haikuwa hitaji la msingi. Pesa hiyo ingetumika kuboresha na kuongeza huduma za matibabu Bugando.
Tunaweka huduma specialized, kama hospitali teule, rufaa au ya Taifa, ili kuondoa malalamiko juu ya upendeleo na kuwabagua watu, ni laza tuwe na vigezo vinavyotuongoza. Kwa mfano:
1) Kila Kanda iwe na jiji moja, hospitali moja teule na uwanja mkubwa wa ndege
2) Kila mkoa uwe na hospitali moja ya rufaa, uwanja wa ndege wa kati na shuoe moja ya watoto wenye uwezo mkubwa kimasomo, ambayo wanafunzi waje, wa mkoa husika, hawatazidi 10%.
3) Kuwepo na hospitali 2 za Taifa, na viwanja viwili vya kimataifa (Dar na Dodoma)
4) Kila wilaya iwe na airstrip, hospitali 1 ya wilaya, na chuo kimoja cha VETA.