Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu, tukashiriki kutoa maoni, majirani wameikataa yao na mpaka sasa wapo kwenye maandamano. Tuchukue somo kwao, kama hatujailewa basi na ijulikane.
Nimeambatisha Muswado huo hapo chini kwaajili ya mapitio.
TAARIFA KWA UMMA
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti imepanga kupokea maoni ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2024, (The Finance Bill, 2024) kwa mujibu wa Kanuni ya 97(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Februari 2023.
Mkutano wa kupokea na kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) utafanyika kuanzia siku ya Jumapili tarehe 23 Juni, 2024 hadi Jumanne tarehe 25 Juni, 2024. Majadiliano hayo yataanza saa 4:00 asubuhi katika Ukumbi wa Piusi Msekwa, Ofisi ya Bunge Jijini Dodoma.
Kamati inawaalika watu wote wenye maoni kuhusu Muswada huo kufika na kuwasilisha maoni yao kabla haujapelekwa katika hatua nyingine.
Vilevile itapokea maoni kwa njia ya posta au Barua pepe kwa anuani ifuatayo:-
Katibu wa Bunge,
Ofisi ya Bunge,
Mtaa wa Makole
S.L.P. 941
41105 DODOMA
Barua pepe: cna@bunge.go.tz na kamati@bunge.go.tz
Muswada huo pia unaweza kupakuliwa katika tovuti ya Bunge, www.bunge.go.tz. Aidha, unashauriwa kuwasilisha jina lako kupitia barua pepe tajwa endapo utaenda kuwasilisha maoni yako kwa kuzungumza kwa ajili yah atua zaidi.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge,
S.L.P 941,
DODOMA.