Serikali yaandaa Mswada wa taratibu za uvunaji na upandikizaji viungo vya binadamu

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel amesema kutokana na kuongezea kwa mahitaji ya upandikizaji wa viungo Nchini, Serikali imeandaa Muswada wa kutunga Sheria itakayoongoza taratibu za uvunaji, utunzaji na upandikizaji wa viungo.

Ameeleza hayo akimjibu Mbunge wa Viti Maalum, Rose Tweve, aliyehoji kuhusu mkakati wa Serikali kuanzisha utaratibu maalum wa kuvuna viungo vya binadamu kama Figo na Moyo kwa ajili ya wenye uhitaji.

Naibu Waziri ameeleza, "Kwa kuwa huduma zimeanza kutolewa, kwa sasa Nchi inatumia miongozo ya kimataifa kusimamia uvunaji na upandikizaji wa viungo".
 
Serikale Wakiruhusu kuuza figo mnistue.

~600millions ni mtaji tosha
 
Naibu Waziri wa Afya, Godwin Mollel amesema kutokana na kuongezea kwa mahitaji ya upandikizaji wa viungo Nchini, Serikali imeandaa Muswada wa kutunga Sheria itakayoongoza taratibu za uvunaji, utunzaji na upandikizaji wa viungo.

Ameeleza hayo akimjibu Mbunge wa Viti Maalum, Rose Tweve, aliyehoji kuhusu mkakati wa Serikali kuanzisha utaratibu maalum wa kuvuna viungo vya binadamu kama Figo na Moyo kwa ajili ya wenye uhitaji.

Naibu Waziri ameeleza, "Kwa kuwa huduma zimeanza kutolewa, kwa sasa Nchi inatumia miongozo ya kimataifa kusimamia uvunaji na upandikizaji wa viungo".
Naunga mkono muswada huo, naona itakua tu mtu akifa viungo vake muhimu vinavoweza kuchukuliwa na nimuhimu kwa watu walio hai kupandikiziwa, vivunwe tu!
 
Si sawa.Itachochea mauaji ya watu wasio na hatia ili tu wapate viungo.
 
Huo ni utaratibu wa lazima na unafanywa na wizara ya afya kuwa maiti ni lazima inyofolewe viungo bila ridhaa yake au jamaa zake, na hivi viungo vinaenda kuhifadhiwa kwenye benki ya viungo
 
Hii hatari
 
Kwani anaweza kufa mtu alafu viungo vyake vikawa vinafanya kazi?maana nlizani mtu akifa na cells zake na organ zake huwa zimefeli
 
Halafu wafanye bure maana wakiweka hela tu basi polisi wajiandae kupokea kesi lukuki mixer upelelezi humohumo Kuna mirushwa visa na mikasa vitakuwa vingi.
 
Huko ni kuikosea heshima maiti
Heshima inahitajika kwa Mungu, malaika na binadamu, na huruma inahitajika kwa wanyama na binadamu. Sasa MAITI inavo chomwa na kuzikwa ardhini na kubeza kaburini hapo inahishimiwa? Mimi ninavoona mtu Akira viungovake vinavoonekana vitasaidia waliohai kuliko kuzikwa na kuozea kaburini, inyofolewe kwa manufaa ya walio hai.
 
Back
Top Bottom