Serikali yaanza kusambaza Katiba inayopendekezwa

Serikali yaanza kusambaza Katiba inayopendekezwa

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Serikali imeanza kusambaza nakala milioni mbili za Katiba Inayopendekezwa nchini kote ili kuwawezesha wananchi kuisoma na kushiriki katika Kura ya Maoni iliyopangwa kufanyika tarehe 30 Aprili mwaka huu.

Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro amesema leo (Jumatano, Februari 11, 2015) jijini Dar es Salaam kuwa kati ya nakala hizo zilizochapwa jijini Dar es Salaam, nakala 1,800,000 zinasambazwa Tanzania bara na nakala 200,000 zinasambazwa Tanzania Zanzibar.

Kwa mujibu wa Waziri Migiro, hadi kufikia jana (Jumanne, Februari 10, 2015), jumla ya nakala 707,140 zilikuwa zimesambazwa katika mikoa 12 ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ambayo imepata nakala 200,000 na kuwa kazi hiyo inaendelea vizuri na inatarajiwa kukamilika katika muda mfupi ujao.

Mikoa hiyo na nakala ziliozosambazwa katika mabano ni Katavi (15,640), Rukwa (27,040), Ruvuma (47,740), Mbeya (78,640), Simiyu (34,840), Mara (52,540), Tabora (58,540) na Kigoma (41,440). Mikoa mingine ni Kagera (54,340), Geita (36,940), Mwanza (57,040) na Pwani ambapo usambazaji umeanza kwa wilaya ya Mafia ambayo imepata nakala 2,400.

“Idadi ya nakala ya Katiba Inayopendekezwa kwa kila mkoa inategemea na wingi wa kata katika mkoa, ndiyo maana baadhi ya mikoa unaona imepata nakala nyingi,” amesema Dkt. Migiro ofisini kwake wakati akiongea na baadhi ya waandishi wa Habari waliotaka ufafanuzi kuhusu hatua iliyofikiwa katika kazi ya uchapishaji na uasambazaji wa nakala za Katiba Inayopendekezwa.

Kwa mujibu wa Waziri Migiro, kuna zaidi kata 3,800 nchini kote na lengo la Serikali ni kusambaza nakala 300 katika kila kata ambazo zitasambazwa kwenye vijiji, vitongoji na mitaa kupitia Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Miji, Manispaa na Majiji.

Kuhusu taasisi za elimu na dini, Waziri Migiro amesema Serikali imepanga kusambaza nakala 658,400 kwa taasisi za elimu, dini, vyama vya siasa na asasi za kiraia na kuwa usambazaji huo utaanza hivi karibuni.

Pamoja na usambazaji huo, Waziri Migiro amewakumbusha wananchi ambao bado hawajapata nakala za Katiba Inayopendekezwa, kuisoma kupitia tovuti ya Wizara ya Katiba na Sheria (Karibu Wizara ya Katiba na Sheria) na tovuti ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (www.agctz.go.tz)
 
wana bodi nimepita mahali na nikathibitishiwa kuwa Serikali itaanza kusambaza Nakala 2,000,000 za Kitabu cha Chenge. Nimejulishwa na mamlaka kuwa kila mkoa utapata nakala 300! Nimerajibu kupiga vijihesabu vyangu hasa kwa mkoa Kilimanjaro ambao unakadiriwa kuwa na watu takribani milioni tatu nikakutana na hiki kioja kuwa uwiano wa kitabu ni 1:10,000

nikajaribu na Jiji la dar es Salaam lenye watu takribani milioni 5 nikakuta uwiano wa 1: 17,000

Muda wa kusoma na kuamua kupiga kura ni siku kama 48 zimebaki. tutaazimana lini mpaka kitufikie wote ?

nawasilisha
 
Waliotoa maoni kwenye tume ya walioba ni takribani laki tatu, watanzania tulilizia kwamba hayo ndo maoni ya watanzania wote, leo hii sisi wenyewe tunadai nakala milioni mbili hazitoshi ni chache, swali langu la msingi je ni kweli maoni yaliyotolewa na watu laki tatu kwa niaba ya watanzania yalikuwa ni maoni ya watanzania wote? kama jibu ni ndio basi tukubaline kwamba nakala millioni mbili watakao zisoma watawaelimisha na wengine na kwa hiyo nakala hizo ni nyingi, na pongezi kwa serilikali kuwaelimisha watu million mbili kuliko tume iliyokusanya maoni kutoka kwa watu laki tatu yakawa ya watz wote.
 
profilepic44327_13.gif
 
mi bado haijaniingia akili kwenye hotuba ya mh.p kama kweli wanania ya dhat watanzania wote wailewe? cna hakika
 
Hapo hesabu zimekushinda kwani? Kifupi nobody is serious

walau wangechapisha nakala mil.15 kwa hesabu za kila na nakala moja wasome wa watanzania wa 3 lakin takwim hz katiba moja itasomwa na watanzania 23 yan ni zaid ya kaya au nyumba 5 kwa katiba moja duh hali ni mbaya sana
 
Kuna means nyingi za kupata habari kwa mwenye kuhitaji...hata zingechapishwa mara mbili ya idadi ya watu waliopo kama hatupo serious kutaka kujua contents haisaidii kitu! Kwa hiyo kama hoja yako ni kutaka kuchapishwa nakala sawa na idadi ya watanzania siungi mkono hoja!
 
Serikali haikuwa na bajeti ya kuandaa Katiba Mpya. Kwa kulazimisha tu, serikali imekosa kujiendesha baada ya kutumia hela katika mambo hayakuwepo.

Sasa hela kuchapisha hizo katiba watapata wapi!!

Ndo yanayokea hata kwenye Daftari ya Wapiga Kura.
 
Kimsingi Katiba Mpya haikuwa katika ilani na wala si sera kabisa....ugumu uko hapo.
 
Kwa katiba hilo ni tatizo. Lakini kwa upande wa rasimu ya katiba mpya serikali imejitahidi kusambaza nakala na kuweka soft copy kwenye Google playstore.
 
mi bado haijaniingia akili kwenye hotuba ya mh.p kama kweli wanania ya dhat watanzania wote wailewe? cna hakika

Sasa wewe ukiipata moja mtolee kopi ambae hajapata na inahihitaji, unangoja kufanyiwa kila kitu?

Kumbuka si wote wenye kuhitaji hayo makaratasi, siku hizi hata ukiwa na simu tu unaingia mtandaoni, kuna katiba zimezagaa za elektroniki mtandaoni, ya nini ubebane na mikaratasi? Fikiri.
 
walau wangechapisha nakala mil.15 kwa hesabu za kila na nakala moja wasome wa watanzania wa 3 lakin takwim hz katiba moja itasomwa na watanzania 23 yan ni zaid ya kaya au nyumba 5 kwa katiba moja duh hali ni mbaya sana

Wangapi kati ya hao Watanzania ni watoto wadogo? wangapi wasiojuwa kusoma? wangapi wasio na shida na kusoma katba na yoyote iwayo kwao ni sawa tu? wangapi wenye access ya mitandao na hawahitaji kuwa na katiba ya makaratasi?

Mimi hiyo ya mikaratasi hata ukinilazimisha siitaki. Ya elektroniki iko hapa: http://www.tanzania.go.tz/home/pages/8

Hizo zilizochapwa tu, ngoja siku mbili tau kama hujaona zinafungiwa vitumbuwa.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Wangapi kati ya hao Watanzania ni watoto wadogo? wangapi wasiojuwa kusoma? wangapi wasio na shida na kusoma katba na yoyote iwayo kwao ni sawa tu? wangapi wenye access ya mitandao na hawahitaji kuwa na katiba ya makaratasi?

Mimi hiyo ya mikaratasi hata ukinilazimisha siitaki. Ya elektroniki iko hapa: Tovuti Kuu ya Serikali: Katiba

Hizo zilizochapwa tu, ngoja siku mbili tau kama hujaona zinafungiwa vitumbuwa.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?

mwisho wa siku kura ni big noooooooooooo
 
Ujinga hauwezi somewa
 
Sasahivi ni Kidigitali bhana. Yanini kutembea na mzigo wa mjikaratsi? Rasimu unazipata kwenye play stote. Katiba inayopendekezwa ipo ktk pdf. Thats y unaambiwa JISMARTIFONISHE!
 
Wangapi kati ya hao Watanzania ni watoto wadogo? wangapi wasiojuwa kusoma? wangapi wasio na shida na kusoma katba na yoyote iwayo kwao ni sawa tu? wangapi wenye access ya mitandao na hawahitaji kuwa na katiba ya makaratasi?

Mimi hiyo ya mikaratasi hata ukinilazimisha siitaki. Ya elektroniki iko hapa: Tovuti Kuu ya Serikali: Katiba

Hizo zilizochapwa tu, ngoja siku mbili tau kama hujaona zinafungiwa vitumbuwa.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?

mkuu usiseme ujinga! yan kund la kulitoa hapo ni watoto pekee dunia ya saiz unaweza ukazunguka kutwa nzima na usikutane na mtu asiyejua kusoma kiukwel kuna improvement ktk elim
 
walau wangechapisha nakala mil.15 kwa hesabu za kila na nakala moja wasome wa watanzania wa 3 lakin takwim hz katiba moja itasomwa na watanzania 23 yan ni zaid ya kaya au nyumba 5 kwa katiba moja duh hali ni mbaya sana

Hiyo mil 45 ni pamoja na wasiojua kusoma wala kuandika.Na mil 2 ndo Watanzania wanaofikrika angarau kuwa na akıli ya kusoma na kuelewa document ya kisherıa.Ndo mana watu wanapenda taasisi za kıtaalam zısaıdıa kuufafanulia umma.
 
Back
Top Bottom