Serikali yaanza maboresho ya machinjio ya Nyama Wilayani Uyui (Tabora)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Baada ya Mwanachama wa JamiiForums.com kulalamikia kuhusu Mradi wa Machinjio uliopo Goweko akidai umekwama kuendelezwa licha ya fedha za walipa kodi takribani Shilingi Milioni 25 kutumika, hatua zimeanza kuchukuliwa.

Malalamiko ya member ~ Haya machinjio ya Nyama Wilayani Uyui (Tabora) ni hatari kwa Afya

Wakazi wa karibu na eneo hilo wameshuhudia mchakato wa kufyeka kwa nyasi zilizokuwepo awali pamoja naa kutengeneza sehemu ambazo zilianza kubomoka.

Mradi huo uliojengwa kwa ajili ya maeneo mbalimbali ikiwemo Kata ya Nsololo, Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora, pia ulikuwa na changamoto ya kukosekana kwa msimamizi wa Afya, hali iliyosababisha Wachinjaji kuwa na maeneo tofauti ya kuchinja jambo ambalo ni hatari kwa afya.

=====

Alipoulizwa kuhusu kinachoendelea hapo, Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Zakaria Mwansansu amesema “Mchakato wa maboresho unaendelea kama unavyoona, tunapokea michango ya Wadau mbalimbali wakiwemo Wananchi katika kutuwezesha kutimiza hilo, hata nyie JamiiForums mnakaribishwa kutuchangia chochote, iwe mfuko mmoja au miwili ya saruji itatufaa.”




Your browser is not able to display this video.

Pia soma ~ Mradi wa Machinjio ambao hautumiki, DC wa Uyui asema wametenga Tsh. 14m hadi 24m kuuboresha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…