Serikali yaanza mazungumzo kwa ajili ya kununua ndege nyingine ya mizigo

Serikali yaanza mazungumzo kwa ajili ya kununua ndege nyingine ya mizigo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema serikali imeshaanza mazungumzo ya namna ya kupata ndege ya mizigo kwaajili ya kubeba mazao ya mbogamboja kuyepaleka nje ili kuwasaidia wakula.

Ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumatano Novemba 13, alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini aliyetaka kujua mkakati wa serikali katika kutafuta ufumbuzi wa masoko ya mazao ya mbogamboga.

“Jimboni Rombo tunalima sana maparachchi na yananunuliwa na wafanyabiashara walanguzi kutoka Kenya, kilimo hiki cha hot culture Kaskazini huko wakulima wanapata hasara kubwa, sasa katika mkakati wa kutafuta masoko ni kwanini tusiangalie uwezekano kama nchi kununua ndege ya mizigo itakayosaidia wakulima wetu nje ya nchi kwasababu mazao haya ya mbogamboga yanakwenda Nairobi na kusafirishwa na ndege za Kenya,” amehoji.

Akijibu hoja hiyo Waziri Kamwelwe amesema serikali imeshafanya mazungumzo juu ya suala hilo na kwamba wana mpango wa kuanza kukodisha ndege kwaajili ya kusafirisha mazao hayo na minofu ya samaki kutoka Mwanza.

“Tayari tuna miezi mitatu tulishaanza kujadiliana kuhusiana na jinsi ya kupata ndege ya mizigo kwaajili ya kubeba mazao ya hot culture Uwanja wa Ndege wa Songwe pamoja na minofu ya samaki kutoka Mwanza kwahiyo tutaanza na kukodi ndege kwasababu tuna changamoto ya mzigo wa kutoka Europe kuja huku lakini kutoka hapa kwenda kule mzigo upo,” amesema Kamwelwe.

Naye Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, amesema serikali imekuwa ikihamasisha wakulima na wadau wengine kuongeza uzalishaji wa zao la parachichi hususan aina ya hass, kutekeleza mkakati wa kuainisha maeneo yote yanayofaa kwa kilimo hicho nchini pamoja na kuongeza uzalishaji wa miche ya maparachichi aina ya hass na kuilinda ili isiharibiwe na aina nyingine za mapachichi.
 
Ndege za mizigo kwa Tz ni Bingo pia kiasi furani itachochea kilimo
 
Ikinunuliwa watasema ,,hatuhitaji ndege”, wakati anayeiomba ni CHADEMA na anaona umuhimu wake.
Inaonekana uwezo wako wa kuchambua mambo ni mdogo. Huyu kaomba soko la mazao yao, mwingine kakimbilia kununua ndege. Ndege bila kuwa na soko unafikiri ni suluhu la mkulima. Selasini kaomba serikali itafute masoko ya mazao ya wakulima ya ndege yanakuja baada ya kupata soko
 
yaani wewe ndiyo mak***lio kabisa ushaambiwa kunasoko europe na huko kuna mizigo ya kuja huku lakini shida usafirishaji aliyekuambia hakuna soko ni nani chadema sijui mmelogwa na nani?
 
Ikinunuliwa watasema ,,hatuhitaji ndege”, wakati anayeiomba ni CHADEMA na anaona umuhimu wake.
We mtu kuulizs tu hivyo amehitaji denge jamaa kauliza mkakati na sio other mbona hata huko marekani wanalima kisasa zaidi na sana sana kutushinda hata sisi tunaolima mboga za majani kwenye mito yenye kemikali

Wanataka yaende wapi labda angesema wanatafuta njia mbadala na tekinolojia iitakayo yafanya yakaee muda mrefu

Ndege ni ujinga tu
 
Jamani nyie CCM siendi mnaimba kuwa Maendeleo hayana chama sasa imekuwa chadema inaomba ndege?
huyo hajaomba ndege ila alikuwa hajui hata hayo mazao yatafikaje kwenye soko yaani ulaya sijui chadema wanajuwa wanaweza kupeleka hayo mazaokwa miguu wakiambiwa soko lik sehemu ? hawanaga hata plani halafu ndyo wanataka nchi hawahawa?
 
Mazungumzo ya nini, si mnunue tu? Kwani hizo zingine si mlinunua tu baada ya kupata ushauri kutoka kwa Kagame!
srilkali haikurupiki kama watu wa chadema mnavyofanya lazima ifanye mazungumzo si unaona wamekurupuak tu dj katoka usingizini kawaambia tususie uchaguzi? hoplesss kabisa cdm
 
Inaonekana uwezo wako wa kuchambua mambo ni mdogo. Huyu kaomba soko la mazao yao, mwingine kakimbilia kununua ndege. Ndege bila kuwa na soko unafikiri ni suluhu la mkulima. Selasini kaomba serikali itafute masoko ya mazao ya wakulima ya ndege yanakuja baada ya kupata soko

Imeandikwa humo ,, ... kwa nini tusiangalie kama nchi kununua ndege ya mizigo,...” - Selasini MB ( chadema)!
 
We mtu kuulizs tu hivyo amehitaji denge jamaa kauliza mkakati na sio other mbona hata huko marekani wanalima kisasa zaidi na sana sana kutushinda hata sisi tunaolima mboga za majani kwenye mito yenye kemikali

Wanataka yaende wapi labda angesema wanatafuta njia mbadala na tekinolojia iitakayo yafanya yakaee muda mrefu

Ndege ni ujinga tu

,, kwa nini tusiangalie uwezekano wa kununua Ndege ya mizigo” - Selasini Mbunge chadema.

Sasa nifafanulie alichomaanisha kama ukipenda/weza.
 
Tutanunua ndege ya mizigo na huku mnabana kuongeza soko la nje kwa kupeleka matunda na mbogamboga
Kuna tatizo kwenye mfumo mzima wa export na hawataki kuliongelea kabisa
Angalia wenzetu Jirani wanavyochangamkia fursa za ulaya na uarabuni kwa kutuma kila siku mboga
Na sisi hata pilipili ukitaka kutuma nje utazungushwa mpaka mtaji ukate
Wake up guys
 
Inaonekana uwezo wako wa kuchambua mambo ni mdogo. Huyu kaomba soko la mazao yao, mwingine kakimbilia kununua ndege. Ndege bila kuwa na soko unafikiri ni suluhu la mkulima. Selasini kaomba serikali itafute masoko ya mazao ya wakulima ya ndege yanakuja baada ya kupata soko

Wewe ndo hujui unachoongea, rudia kusoma uone kasemaje badae ili uelewe kasema hivi kama inchi itafute uwezekano wa kuwa na ndege ya mizigo, kwa hiyo kaona umuhimu wa hiyo ndege pamoja na soko.
 
Tatizo mizigo ya kuja Tz ndo shida. Kenya wana mizigo mingi inayokuja na kutoka
 
Kama mchakato wa kununua ndege ya mizigo umeishaanza sidhani kama kuna ubaya tukishauri aina ya ndege itakayotufaa kubeba mizigo ya kiraia na pale itakapohitajika mizigo ya kijeshi. Nashauri inunuliwe McDonnell Dougras10....DC*KC-10.💪
Screenshot_2019-11-13 KC-10 Extender (2151957820) - McDonnell Douglas DC-10 - Wikipedia.png
 
Back
Top Bottom