Serikali Yaanzisha RRI Kupambana na GBV na Femicide Western Kenya

Serikali Yaanzisha RRI Kupambana na GBV na Femicide Western Kenya

Ikariiah

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
287
Reaction score
314
Serikali imeanzisha Rapid Results Initiative (RRI) ya miezi 3 katika Ukanda wa Magharibi, yaani, Western Kenya, ikiwa na lengo la kuharakisha hatua dhidi ya ongezeko la matukio ya unyanyasaji wa kijinsia (GBV) na mauaji ya wanawake (femicide).

Mpango huo umeanzishwa na 'State Department for Gender and Affirmative Action' huku Serikali ikitaka taasisi mbalimbali kutosubiri taratibu za kawaida pekee, bali zifanye kazi kwa kasi ndani ya kipindi hicho cha miezi 3.

Fahamu kuwa kati ya Januari na Septemba 2026, Western Kenya iliripotiwa kuwa na kesi 3,191 za GBV, zikiwemo ubakaji, aina nyingine za ukatili. Kwa hiyo, swali si kama tatizo lipo. Lipo! Swali kubwa ni nini kitabadilika ndani ya hizo siku 90?

Mpango huo unadhamiria yafuatayo:

1)Polisi kuharakisha ukamataji na uchunguzi wa wahusika.
2)Mahakama kuharakisha usikilizwaji wa kesi na kupunguza ucheleweshaji usio wa lazima.
3)Sekta ya afya kuimarisha mwitikio kwa waathirika.
4)Shule kutoa elimu kuhusu GBV na namna ya kuripoti.
5)Viongozi wa dini na jamii kushiriki katika kuzuia ukatili na kuhamasisha kuripoti.
6) Wafanyakazi wa Jamii, yaani, Community Health Promoters kujengewa uwezo wa kutambua na kuripoti visa.

Aidha, Kamanda wa Polisi Ukanda wa Western George Seda amesema Polisi wanaendelea kukabiliana na pombe haramu na dawa za kulevya, akihusisha baadhi ya visa vya GBV na matumizi ya vitu hivyo.

Sasa RRI ipimwe kwa kutumia vigezo gani?

Ikumbukwe sio mara ya kwanza kwa Serikali kuanzisha RRI ya sampuli hii. Mpango kama huo ulizinduliwa katika Ukanda wa Kati(Central Kenya) mwezi Mei mwaka huu ukiwalenga pia SGBV, utekaji wa watoto na mauaji.

Kwa hiyo, hii si habari ya “serikali imezindua mpango” pekee.
Ni ahadi yenye deadline. Je, Siku 90 zinatosha Serikali kuonyesha kama RRI imeleta kasi halisi kwenye uchunguzi, ulinzi, huduma kwa waathirika na haki mahakamani au kama tutasubiri uzinduzi mwingine baada ya miezi mitatu?

Wewe unafikiri ni matokeo gani tunapaswa kudai kutoka kwa serikali ili kujua RRI imefanikiwa baada ya siku 90?
 
Back
Top Bottom