Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,194
- 911
Sekta ya umwagiliaji Tanzania imeendelea kukua kwa kasi, huku eneo linalohudumiwa na kilimo cha umwagiliaji likiongezeka kutoka hekta 561,383 mwaka 2020 hadi hekta 727,281 mwaka 2022, na kufikia hekta 983,466 mwaka 2025 ongezeko la takriban asilimia 75 ndani ya miaka mitano. Serikali inalenga kuongeza eneo hilo hadi hekta milioni 1.67 ifikapo mwaka 2028, hatua itakayosaidia kuongeza uzalishaji wa mazao, kuimarisha usalama wa chakula na kuongeza kipato cha wakulima.