The Supreme Conqueror
JF-Expert Member
- Feb 13, 2017
- 458
- 1,280
Pwani
Serikali kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeendelea kuboresha na kufanya matengenezo ya miundombinu ya barabara katika mkoa wa Pwani ili kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji kwa wananchi.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila alipotembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali mkoani humo.
“Hapa Utete ambapo naona ujenzi unaendelea vizuri na tumesisitiza barabara ijengwe kwa ubora na kumalizika kwa wakati kwa manufaa ya wananchi, lakini pia tumetembelea ujenzi wa daraja la Muhoro ili kuona maendeleo yake kwani daraja lilikamilika litasaidia kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji z
kwa wananchi", alisema Mhandisi Mativila.
Pia, Mhandisi Mativila amewataka wasimamizi wa miradi hii kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kwa viwango kwa ajili ya manufaa ya wananchi.
Meneja wa TARURA Mkoa wa Pwani, Mhandisi Leopold
Runji ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa fedha za ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara mkoani humo kwani wameweza kutatua kero za wananchi na kuwaletea maendeleo.
Alisema kuwa daraja la Muhoro ambalo awali lilijaa maji, sasa limepata ufumbuzi kwani wanaamini baada ya matengenezo kuisha wananchi wataendelea kutumia barabara bila matatizo.
Baadhi ya wananchi waliipongeza Serikali na kusema kukamilika kwa daraja hilo kutawasaidia wananchi kuvuka kwa urahisi na kuendelea na shughuli zao za kiuchumi na kijamii.