lady j
Member
- Mar 22, 2013
- 78
- 27
Ni kama vile Serikali imeamua kupuuzia mustakabali wa Elimu ya Tanzania licha ya kelele zinazopigwa kila siku kufuatia kuyumba kwa elimu ya nchi hii,safari hii serikali imewahadaa walimu kwa kushindwa kutekeleza ahadi yake kuwa ingewalipa walimu waliorekebishiwa madaraja mishahara mipya kuanzia mwezi April mwaka huu kulingana na madaraja waliyopandishwa, inasikitisha kuona nikiwa mmojawapo wa walimu hao mshahara wa mwezi huu umekuja bila ya hayo marekebisho. Huu ni mzaha na kuendeleza kejeli dhidi ya walimu kwa jambo ambalo serikali yenyewe ilihaidi tena kwa njia ya barua.