Elections 2010 Serikali yafadhili kampeni za CCM

Naomba mtu anieleze nini maana ya neno kuchakachua...ni ku-dilute au kuchanganya vitu viwili tofauti au hasa nini maana yake?
Kufanya deal ili upate faida bila kutoa jasho. (Forgery/ falsification)
 
Gazeti la Mwanahalisi la leo (August 11-17) limetoa taarifa ya Ikulu kufadhili kampeni za CCM kwa kuchapisha fulana na picha ya Rais. Sijui hii ni EPA nyingine, sina uhakika. Naomba tujadili.....

Mzeewapori
 
Kufanya deal ili upate faida bila kutoa jasho. (Forgery/ falsification)



Thanks! Kwa vile mara ya kwanza nilisikia juu ya mafuta nikafikiri ni kuchanganya (miscible ingredients). Sasa leo nikaona linatumika kwenye mambo ya Fedha. Natumaini umenipa jibu sahihi.
 
Mafisadi wanazidi kuumbuka. Naomba mwenye soft copy aturushie tupate kujadili kwa kina.
 
duh,sasa wenye datda watoe, wengine tuko mbaliiiiiii
 
... Haya, Mr Hosea, kama una ubavu, ingia kwenye hili na tutarajie watu wanasimama kizimbani kabla ya October 31. Huna ubavu.


jamaa yupo kwenye nafasi ya utii kwa bosi wake hawezi kumshitaki na si kosa lake.
wenye uwezo huo ni wananchi. mwenye macho haambiwi tazama.
 
Nahisi mhariri atakuwa na bonge la back up yaani" evidence " kama hana hapo sasa yataibuka mengi.
 
WE NEED THE CHANGE IN OUR COUNTRY, THE CHANGE THAT WILL PUT OUR COUNTRY IN THE WORLD, siyo kama sasa tunajulikana kwa mlima kilimanjaro tu, wakato mwingine kujitambulisha mpaka uanzie kenya jamani! Napata shida mimi hapa nilipo. watu hawaijui Tanzania wanaijua Kenya tu, hapa ni kupiga chini CCM harafu warudishe pesa yote ya umma.

Hakuna kuonea aibu hapa.
 
Mungu amesikia kilio cha Watanzania milioni 40 wanaokandamizwa na manyangau wachache, sasa yale yote waliyofanya sirini yatawekwa peupe ili watanzania wafanye maamuzi sahihi.Naamini kabisa kuwa kuanikwa kwa uovu wa majambazi hawa ni mpango mahsusi wa Mungu kuwakomboa watu wake. Kila lenye mwanzo ni lazima liwe na mwisho. GLORY TO GOD
 
duh - kula kona kwanuka uvundo....guys we need to do an emergency restructuring of this junk system asap kwa sababu imeprove failure
How to go about it - VOTE YES to DR. Slaa Come October 31st. ukifanya hivyo utakuwa umeamua kubadilisha mfumo huu uliopo. vinginevyo basi utegemee mengi zaidi ya haya miaka 5 ijayo, njaa, mateso, ufisadi na inawezekana hata na sisi wananchi tukabinafishishwa on the process.

Mabadiliko ndiyo itakuwa solution na hayo yote, lazima watanzania tuamke na tukubali kufanya changes, tunakwisha.
 
Hili ni bonge la muvie.
Tofauti ya muvi hii na ile ya EPA ni kwamba muvi hii imegundulika kabla hata ya muda wa kampeni.
wakati ile ya EPA iligundulika baadae watu wakiwa tayari wapo madarakani.
Imefika kipindi kwa Watanzania kusimama na kusema 'ENOUGH IS ENOUGH'
 

Naomba mji!
 

Hili siyo jipya ndugu maana kila mwaka wakati wa uchaguzi mambo huenda hovyo kila sehemu. eti hela zimeenda kwenye uchaguzi either direct or Indirect. So siyo ajabu sana. so far., Serikali ndo CCM ambayo inagombea pia. Kwahiyo hata ikaficha kuwa hakuna mkono wake, basi utakuwepo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…