Elections 2010 Serikali yafadhili kampeni za CCM

mmhhhh-cna comment,machozi tu yananitoka, nawalilia wale wanachi walipo vijijini amabo hawajui lini watapata hata maji safi.eee mola mwenye huruma, uliyeumba mbingu na vyote vilivyomo,tusaidie waja wako.
 
hivi jamani mnasubiri tu CCM iendeleee kukaa madarakani kwa madudu kama haya. Sie wengine tunavyohenyeka maisha wengine wanatafuna kodi zetu kama pesa zao. Ama hakika machozi yananitoka kwani huu ni ufisadi mtupu
 
Kama nitachulia labda kwamba hii habari ni miongoni mwa mabomu 20 ambayo Dr. Slaa alisema wakati wake bado; hayo 19 yaliyobaki yatakuwa na taswira gani hasa katika thamani ya kifedha?! Kweli ndo maana NEC imetoa mwongozo wa maadili unaopunguza uhuru wa kuya-blast haya madudu jukwaani. Inaudhi, Inauma saana. Nina hakika sote tunaoishi kizazi hiki watoto na wajukuu zetu watatulaani sana tusifanya mapinduzi kuondoa huu udharimu
 
Well kabla hata hatujaingia ndani ya huu upupu, hivi sisi tutakuwa malimbukeni mpaka lini? Yaani hata picha zinachapishwa na kuagizwa nje???????? This is ridiculous!!!!!!!!!!!

And wht a f.c.k, yaani kodi zetu zitumike kuchapisha picha za JK? It seems hawa jamaa wamelewa kabisa na hii rushwa. Maana hawaoni hata aibu!
 
Uchakachuaji ni adulteration, yaani, kubadilisha kutoka kwenye hali moja kuwa hali nyingine. Kwa mfano, mafuta ya dizeli ukiyachakachua na mafuta ya taa, si mafuta ya dizeli tena, kwani ni mchanganyiko.

Kwa upande wa CCM, wanachofanya ni wanachukua kura hewa wanazichanganya na kura halali halafu wanasema kura hizi ni za mgombea fulani, jambo ambalo ni wizi, kama kwenye uchakachuaji wa mafuta ya dizeli.

CCM mabingwa kwa uchakachuaji wa kura... zote... za maoni hadi uchaguzi mkuu. Sorry, I mean uchafuzi mkuu!

Lakini kiama cha CCM kiko njiani. Kwani KANU nao si walisema kwamba hawataondoka madarakani? Mbona leo wanaitwa chama cha upinani?

LOL
 
Kweli ukistaajabu ya musa, yaani biashara ya kodi zetu inafanyika waziwazi hawana hata aibu, haya ndiyo mambo ya kufuatilia badala yake eti wanafuatilia Chadema imeanza kampeni mapema.

Nasikia Tambwe alipoulizwa kuhusu serikali kufadhili kampeni za CCM akawatukana waandishi wa habari na mkutano ukavunjika nafuatilia nijue kama ni kweli basi hili nalo ni doa jingine kazi kwao.
 
Duh hiyo habari kwenye attachment ni ya kusomwa ktk moja ya mikutano ya kampeni ikianza na wananchi waelezeze jinsi gani kodi yao inatumika bila ridhaa na kwa manufaa ya mtu binafsi.
 

Hey Doubting Thomas,kwanini usiokoe muda wako kwa kuamini unachotaka kuamini? Hujashikiwa mtutu wa bunduki kulazimishwa kuamini habari husika.Unataka ushahidi wa habari hiyo as if ukishaona ushahidi huo utashawishika kuamini kuwa ufisadi is actually a fact and not fiction.By the way,kwanini usijihangaishe japo kidogo kutafuta nakala ya gazeti husika kisha you make up your mind kama stori ni ya kweli au la.
NB: kwa kukusaidia,kuna pdf attachment ktk post moja hapo juu.I just hope you'll come back to tell us what you think of the story...
 
Salva akikanusha kwenyemagazeti hayohayo utayaamini au utabaki na msimamo wako huohuo? tusiwe jamii ya kuamini kila kiandikwacho kwa kuwa tu kimeandikwa kwenye magazeti

Inavyoonekana wewe ndugu yetu ni wale wale.. Mwandishi ameambatanisha vielelezo unavyo vitaka (vinachapiwa wapi, na kampuni gani na nani mlipaji copy ya profoma invoice sasa Salva alitakiwa kukanusha na kuuthibitishia uma kuwa vielelezo vile si halali ni vya kugushi ili mwandishi atuletee ushahidi zaidi kwani kama kampuni iliyotumika ni ya kimataifa mambo yatakuwa wazi tu.
 
soma habari yenyewe live

Kinachonifurahisha kwenye hii habari ni kwamba Salva ameminywa between a rock and a hard place, in some sense hana uhakika how much info Mwanahalisi wanazo, pia wamepataje, nani amewapa etc. NA HUU NDIYO UANDISHI WA HABARI ZA KIUCHUNGUZI. BIG UP MWANAHALISI. In simple bongo terms jamaa wanawweza kuwa wanafikiria namna ya kumpooza mwanahalisi kwa rushwa but how and who? Na je watakuwa na uhakika gani kwamba jamaa hatatoa kwenye gazeti lake hiyo habari......

I can see kwa mbali if push comes to shovel, CCM itamruka Salva, walivyo wasanii wanaweza hata kujifanya wanaanzisha uchunguzi wa TAKUKURU.

TWENDE MBELE TURUDI NYUMA, tANZANIA IMEOZA NA NI LAZIMA TUANZE UPYA!
 
watumie kila njia lakini wajue dk atawasumbua sana tena sana 2
 
Kuna vitu vinasikitisha na kichefuchefu hivi wadanganyika wenzangu mpaka lini tutaendelea kukumbatia huu uovu wa kodi zetu kuchezewa na baadhi ya wachache watakavyo? na inatokana na jeuri ya chama tawala "hata hao walipa kodi wakijua litapita na wataendelea na mambo yao kama kawaida, nini cha kufanya nafikiri kwa maoni yangu kura yako ndio ya kuondoa udhalimu huu na jeuri iliyopo. MABADILIKO MUHIMU HATA TUKIANZA MOJA POTELEA MBALI
 
Nyambala hama nchi,umelazimishwa kukaa Tanzania.............................?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…