Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Awali, Mwanachama wa JamiiForums.com alidai jengo hilo kubwa la ghorofa ambalo lilikusudiwa kutumiwa kama ofisi na huduma mbalimbali zinazoenda sambamba maendeleo ya soko hilo limetelekezwa na hivyo kuhoji nini kinachoendelea kwa sasa, pia akahoji
Kusoma hoja ya Mwanachama wa JF ~ Soko la Kijichi (Temeke) limejengwa kwa Mamilioni ya mkopo wa Benki ya Dunia lakini halitumiki, nini hatima yake?
UFAFANUZI WA DC
Mkuu wa wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda amesema:
Hatujakaa kimya kuna vikao vinaendelea vya ndani Serikalini kuhusu soko hilo na baada ya muda tutaweka wazi juu ya kinachoendelea lakini kuna mambo mazuri yanakuja na hatujalitelekeza.
Kuhusu masuala ya malipo ya Mkopo hilo zungumza na Mkurugenzi wa Temeke anaweza kukupa ufafanuzi mzuri kwa kuwa ndiye anayesimamia kwa ukaribu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, Elihuruma Mabelya amesema: Tuna mchakato wa kuboresha masoko yote sio hilo la Kijichi pekee.
", kuhusu hilo ambalo umeulizia kuna sababu ambazo zilitolewa na Wasafirishaji na ikawa ngumu kuendeleza mchakato wa soko.
Mpango uliopo ni kuwa tunatarajiwa kufanya mabadiliko ya matumizi ili isiwe soko, hilo litawezekana kwa kutegemea na mwelekeo wa Serikali ambapo mpango huo ukifanikiwa utashirikisha Sekta Binafasi,
Hivyo, kuna mchakato wa vikao na mambo mengine ya Kiserikali yanaendelea ndani kwa sasa kwa kuwa ni lazima tupate hidhini ya Mamlaka husika.
Eneo hilo lipo vizuri kwa mtumizi mengine mbalimbali ikiwemo michezo ya Watoto na mambo mengine mengi.
Tumeshawasiliana na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa jili ya Mawazo yetu ya kubadilisha kwa ajili ya matumizi mengine.
Malipo ya Mkopo
Kuhusu malipo ya mkopo huo ni utaratibu mwingine, na kwa taarifa yako Benki ya Dunia wametupongeza sana kwa kuwa mfano wa kuigwa, kwani wakati inatatumika kama Stendi na Soko kulikuwa na marejesho yanayofanyika kwa wakati.
Pia soma ~ Serikali yasema baada ya miezi miwili itatangaza fursa ya uwekezaji Soko la Kijichi