Serikali yafungua akaunti maalum ya Uhujumu Uchumi

mkiluvya

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2019
Posts
809
Reaction score
729
Serikali imefungua akaunti maalum ambayo watuhumiwa wa uhujumu uchumi waliokiri makosa yao wataweka fedha wanazotuhumiwa kuhujumu, ili kuachiwa huru.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) nchini Tanzania, Biswalo Mganga jana Alhamisi October 3.

DPP hakuna fedha itakayolipwa kwenye akaunti ya mahakama, ofisi ya Taifa ya Mashtaka au Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Ambaye atalipa kwingine huko tusilaumiane, lazima fedha ziende zinapotakiwa kwenda, si mawakili wa Serikali, si watumishi wa ofisi hii au mtu yeyote atakayefanya vitendo vya rushwa tutamvumilia,” amesema

Biswalo amefikia hatua hiyo baada ya kuwepo baadhi mawakili wanaochukua fedha kwa washtakiwa na kusema wanapeleka ofisini kwake ila hawafikishi. Amewaonya kuacha tabia hiyo kwa sababu wanatafuta ugomvi.
 
Kwani utaratibu upoje? Inaweza tokea nipo kitaa nikaona hali ni tete nikaenda kuweka hela kwenye hiyo acc ili nisishtakiwe Au mpaka nishtakiwe kwanza?
 
Tuendelee kuhujumu uchumi,tukikamatwa tunarudisha kwenye akaunti tunakuwa huru.
 
Naona umepigia mstari aya hiyo mkuu inabeba uzito mkubwa
Biswalo amefikia hatua hiyo baada ya kuwepo baadhi mawakili wanaochukua fedha kwa washtakiwa na kusema wanapeleka ofisini kwake ila hawafikishi. Amewaonya kuacha tabia hiyo kwa sababu wanatafuta ugomvi.
 
kwan zikiingia kwenye account ya mahakama kuna tatizo,,,
Halafu na Kwa wenye case za uhujumu uchumi ambao wapo nje Kwa zamana kama kina ndama mutoto ya ng'ombe wao haiwahusu huo msamaha
 
Serikali imefungua akaunti maalum ambayo watuhumiwa wa uhujumu uchumi waliokiri makosa yao wataweka fedha wanazotuhumiwa kuhujumu, ili kuachiwa huru.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) nchini Tanzania, Biswalo Mganga jana Alhamisi October 3.
DPP hakuna fedha itakayolipwa kwenye akaunti ya mahakama, ofisi ya Taifa ya Mashtaka au Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
“Ambaye atalipa kwingine huko tusilaumiane, lazima fedha ziende zinapotakiwa kwenda, si mawakili wa Serikali, si watumishi wa ofisi hii au mtu yeyote atakayefanya vitendo vya rushwa tutamvumilia,” amesema
Biswalo amefikia hatua hiyo baada ya kuwepo baadhi mawakili wanaochukua fedha kwa washtakiwa na kusema wanapeleka ofisini kwake ila hawafikishi. Amewaonya kuacha tabia hiyo kwa sababu wanatafuta ugomvi.
Hata hiyo Ac. Ni hujumu uchumi anaebisha atatuletea mrejesho wa matumizi ya hizo fedha. Nakumbuka kuna wawili walirudisha kwa TRA sasa kwann hao wafunguliwe acc. yao? Nchi yetu wizi utaisha lini sijui!
 
Wasisahau Pia CAG Kuruhusiwa Kukagua Account Iyo Kila Mwaka"
 
Isije ikatokea kama ya Escrow hela ni za umma ama sio za umma ,hela za DPP ni za mafisadi au za Magufuli ...????
 
Wahujumu uchumi account [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]tetehteh .Tutaona mengi
 
Back
Top Bottom