Serikali yafuta ada ya Mitihani kwa watahiniwa wa shule za Serikali

Mnafurahi kufutwa kwa hizo ada? Badala yake inaletwa Tozo ya aina nyjngine halafu mnaanza kulalamika.

Ilitangazwa elimu bure, gharama za maisha zikapanda hasa upande wa matibabu.
Sasa na hii, sijui nini kitatokea.
Kama walivyojifanya wanaongeza mshahara halafu wakaweka TOZO kuitoa mshahara huo benki
 
Mama anaupiga mwingi sekta ya elimu
 
Waliwahi kufanya hivyo 2011 ila 2012 ilirudishwa. Ni suala la muda tu.

Serikali ya kurithi.
Usikalili hii ni Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwaiyo mambo ni tofauti awamu hii haina propaganda
 
Taarifa iliyotolewa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) imesema watahiniwa wa Darasa la 7, Kidato cha 4 na 6 kutoka shule za Serikali hawatolipa ada hizo kuanzia sasa.
Zilikuwa zinaliwa na kale jamaa kalikohamishiwa Loca Gvt, during kazi maalumu ananunua sahani ya chakula kwa 6K per marker anaandika 12K, ukweli hakuna atakayeziona mbingu
 
Serikali sikivu ya chama cha mapinduzi inabagua raia wake kwa mataba ya kodi huyu wa private analipishwa ili iweje??? ni kumkomoa mzazi ama?? ubaguzi wa kipumbavu sana kila wizara imekaa kifala fala sana... kodi mashirika na taasisi binafsi wanakatwa kubwa ajabu bado waje mashuleni tena huu ni upumbavu
 
Napendekeza wafute kwa shule zote, mtihani ni uleule na wanafunzi wote ni watanzania na wazazi wao pia ni watanzania. Hii itapunguza malalamiko yasiyo ya lazima kwa serikali.
 
Mbona haya mambo yapo toka zamani (elimu bure) Kwani kuna watu walikuwa wanalipa.

Hizi janja janja tu msitufanye wajinga.

Mnataka kuonesha umuhimu wa tozo wakati hapo nyuma tozo hazikuwepo na bado hiyo gharama haikuwapo
Sahihi kabisa Kaka...nashangaaa wanajishaua hapa,wanaona watu wajinga[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mbona haya mambo yapo toka zamani (elimu bure) Kwani kuna watu walikuwa wanalipa.

Hizi janja janja tu msitufanye wajinga.

Mnataka kuonesha umuhimu wa tozo wakati hapo nyuma tozo hazikuwepo na bado hiyo gharama haikuwapo
Nimeshangaa sana hata mimi. Ada zote zilifutwa na Magufuri.
Aliyekuwa analipa ada ya mitihani aje hapa.

Waseme walichofuta ni ada ya kidato cha sita tu.
 
Kinafutwa kitu kidogo then kinakuja kuongezwa kitu kikubwa. Anyway mama anaupiga mwingi😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…