Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Hayo yamesemwa leo Agosti 14 , 2024 na Waziri wa Madini Anthony Mavunde wakati akiwasilisha taarifa kwa Kamati ya Bunge Nishati na Madini kuhusu hali ya Usimamizi na Uendelezaji wa Leseni zilizotolewa kwa ajili ya Utafutaji na Uchimbaji wa Madini.
Mavunde amesema kuwa maombi hayo yalifutwa baada ya kubainika kuwa, waombaji hawakuwa na nia ya kupatiwa leseni za utafutaji madini na badala yake walikuwa wameyashikilia na kuhodhi maeneo hayo na hivyo kuwanyima fursa wenye nia ya kuyaendeleza.
Mavunde amesema kuwa, Wizara kupitia Tume ya Madini imeendelea kutoa hati za makosa kwa wamiliki wa leseni kutokana na ukiukwaji wa masharti ya leseni zao kwa mujibu wa Sheria ya Madini Sura 123 ambapo jumla ya leseni 110 za utafutaji madini, leseni 13 za uchimbaji wa kati na leseni 2 za uyeyushaji wa madini zilipewa hati ya makosa.
Awali, akiwasilisha taarifa kwa Kamati ya Bunge Nishati na Madini, Kaimu Katibu Mtendaji Tume ya Madini Mhandisi Ramadhani Lwambo amesema kwa kipindi cha Oktoba 2023 hadi Julai 2024 , Tume ya Madini ilitoa leseni moja ya uchimbaji mkubwa , leseni 20 za uchimbaji wa kati na leseni 7974 za uchimbaji mdogo katika maeneo mbalimbali nchini.