Serikali yafuta vijiji na vitongoji vyote vya wamasai wa Ngorongoro kupitia Amri ya tangazo la Serikali namba 673

Serikali yafuta vijiji na vitongoji vyote vya wamasai wa Ngorongoro kupitia Amri ya tangazo la Serikali namba 673

Heparin

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2021
Posts
242
Reaction score
1,141
AMRI YA MAREKEBISHO YA AMRI YA MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA KATIKA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA WILAYA) YA MWAKA 2024

1. Amri hii itajulikana kama Amri ya Marekebisho ya Amri ya Mgawanyo wa Maeneo ya Utawala katika Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) ya Mwaka 2024 na itasomwa pamoja na Amri ya Mgawanyo wa Maeneo ya Utawala katika Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) ya Mwaka 2019 ambayo hapa imerejewa kama "Amri kuu".

2. Amri kuu inarekebishwa katika Jedwali kwa kufuta kata, vijiji na vitongoji katika Halmashauri za Wilaya ya Ngorongoro, Bahi, Chemba, Kasulu, Kakonko, Hai na Rombo kama ilivyoainishwa katika Jedwali.

Hili ni Tangazo la Serikali namba 673 la Agosti 2, 2024.

Kwa mujibu wa tangazo hili, vitongoji 96 na vijiji 25 vya Ngorongoro vimefutwa.
IMG_20240819_220557.jpg

Pia soma
 
Attachments

Kule ni hifadhini sio makazi ya binadamu,Masai sio wa kwanza kuhamishwa kwenye Hifadhi.Imefanyija hivyo Ruaha,imefanyika hivyo kwenye migodi ya Madini na imefanyika hivyo maeneo mengine kupisha maendeleo.

Kipawa pale Hadi Leo hii watu wanadai fidia lakini Masai wanahamishwa na kulipwa Kila kitu nk nk.

Kwamba Masai ndio spesho sana au? Ngorongoro ni Mali ya Tanzania sio Masai.
 
Hivi,kule kisiwani Zanzibar wale binadamu wanafanya nini kule?Kwa nini wasihamishiwe Shinyanga ili watalii wakione kisiwa hicho kwa uzuri zaidi?Wanatukosesha mapato wale.Zanzibar island(s) is for tourism industry!Zanzibar ni kwa ajili ya uchumi wa kibuluu.
 
Ni muhimu sana wakatii sheria bila shuruti, na ni jambo la maana zaidi wakaepuka ukaidi kwa kurubuniwa kifikra na wanaharakti uchwara au wanasiasa waliofulisika hoja huku wakidanganywa ati sheria na amri hiyo inaweza kubadilishwa 🐒

natoa Rai kwamba,
waondoke maeneo hayo ya hifadhi kwa amani mara moja 🐒
 
AMRI YA MAREKEBISHO YA AMRI YA MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA KATIKA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA WILAYA) YA MWAKA 2024

1. Amri hii itajulikana kama Amri ya Marekebisho ya Amri ya Mgawanyo wa Maeneo ya Utawala katika Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) ya Mwaka 2024 na itasomwa pamoja na Amri ya Mgawanyo wa Maeneo ya Utawala katika Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) ya Mwaka 2019 ambayo hapa imerejewa kama "Amri kuu".

2. Amri kuu inarekebishwa katika Jedwali kwa kufuta kata, vijiji na vitongoji katika Halmashauri za Wilaya ya Ngorongoro, Bahi, Chemba, Kasulu, Kakonko, Hai na Rombo kama ilivyoainishwa katika Jedwali.

Hili ni Tangazo la Serikali namba 673 la Agosti 2, 2024.

View attachment 3074381

Pia soma>> Wamasai wa Ngorongoro watoa tamko kunyang'anywa haki ya kupiga kura 2024
ni muhimu sana wakatii sheria bila shuruti, na ni jambo la maana zaidi wakaepuka ukaidi kwa kurubuniwa kifikra na wanaharakti uchwara au wanasiasa waliofulisika hoja huku wakidanganywa ati sheria na amri hiyo inaweza kubadilishwa 🐒

natoa Rai kwamba,
waondoke maeneo hayo ya hifadhi kwa amani 🐒
 
Back
Top Bottom