BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, Uledi Mussa amesema Vikosi hivyo vimeondolewa ili kuhakikisha kunakuwa na Haki katika ukusanyaji mapato nchini.
Amesema TRA inataka watu walipe Kodi bila Shuruti na hivyo Mamlaka hiyo imeagiza Maofisa wake wakusanye kodi bila matumizi yoyote ya nguvu.
Utaratibu wa Ukusanyaji Kodi kwa kutumia Vikosi Kazi ulilalamikiwa kuwa na ukiukaji mkubwa wa Sheria na Haki za Binadamu katika utekelezaji wake.
====================
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Uledi Mussa amesema kwa sasa wanakusanya kodi kutoka kwa wafanyabiashara bila kutumia mabavu.
Amesema kitengo cha 'task force' kilichokuwapo huko nyuma na kutumika kukusanya kodi wamekiondoa.
Mussa amesema hayo leo Jumanne Novemba 15, 2022 katika kikao baina ya TRA na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) jijini Dar es Salaam.
"Kwa sasa tunakusanya mapato bila mabavu. Waachane kabisa kabisa na matumizi ya manavu. Tunataka walipa kodi wajisikie vizuri kabisa. Hatuna tena Taska Force (kikosi kazi)," amesema
Mwenyekiti huyo amesema,"walipa kodi, tunawaangalia kwa macho mawili kuhakikisha wanaendelea kufanya biashara zao ili wawe walipa kodi siku zijazo."
Amesema hatua hiyo imewezesha ukusanyaji wa mapato umeongezeka akitolea mfano mapato ya Septemba yamevuka lengo badala ya kukusanya Sh6.2 trilioni wamekusanya Sh6.3 trillion.
Katika kikao hicho, wahariri wameuliza maswali mbalimbali likiwemo umuhimu wa TRA kuwaomba radhi wale wote walioumizwa na kikosi kazi hicho.
Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipa Kodi, wa TRA, Richard Kayombo amesema,"kuna mengi yamefanyika nyuma ya pazia kuhakikisha yanakaa sawa. Kwa wale tuliokaa nao mmoja mmoja tumewezesha mambo kwenda sawa."
Amesema mazingira ya sasa na huko nyuma yalikuwa tofauti hivyo wanajitahidi kuweka mazingira rafiki zaidi kwa kila mmoja kufurahia anachokifanya.
Naye Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile amewapongeza TRA kwa kuamua kukutana na wahariri kwani ni inaingesha hali ya kushirikiana ili kuhakikisha dhamira ya elimu kwa wananchi kuhusu kulipa kodi inafanikiwa.
"Pamoja na malalamiko yote, tunawapongeza sana, kwa sasa hatujaona makufuri yakifungwa kwa wafanyabiashara, hili ni jambo zuri," amesema
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa TEF, Bakari Machumu amepongeza jitihada zinazofanywa za kuweka mazingira mazuri ya kulipa kodi hilo linatia moyo.
Machumu ambaye pia ni Mkurugenzi Mtebdaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) amesema, kila mmoja akiwa na uelewa wa pamoja na shirikishi hata mapato yataongezeka.