Serikali yafuta vyuo kumi

Serikali yafuta vyuo kumi

mpalu

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2010
Posts
2,521
Reaction score
874
Philipo-Mulugo.jpg



Naibu Waziri wa Elimu, Phillip Mulugo

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imekunjua makucha yake kwa kutangaza kuvifuta vyuo 10 ambavyo havikusajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) .

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Philip Mulugo, alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaama mbele ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na kuongeza kuwa kufutwa kwa vyuo hivyo ni kutokana na kutokufuata utaratibu wa kusajiliwa.

Alivitaja vyuo hivyo ni Media and Research Center, Vision Hotel and Tourism College, East Africa College of Hospitality and Tourism, The Africa Institute of Business Management na Aspiration Training Center, vyote vya Dar es Salaam.

Vingine ni Dar es Salaam School of Hair Design, Media and Values Training Institute na Information Technology Training Center vya Dar es Salaam. Pia alikitaja Chuo cha Morogoro School of Medical Sciences cha Morogoro.

Katika hatua nyingine, Mulugo alikiri kuwa kuna upungufu katika kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kupitia bodi ya mikopo.

Alisema kuna changamoto nyingi zinazoikabili bodi hiyo zikiwamo urejeshwaji wa mikopo kwa wanafunzi waliomaliza chuo, mfumo wa utoaji wa mikopo, ufinyu wa bajeti na makosa yanayotokana na wanafunzi kukosea kujaza fomu za mikopo


SOURCE:PAPARAZI: HIVI NDIVYO VYUO KUMI{10} VILIVYOFUTWA NA SERIKALI....vitambue hapa

MAONI YANGU: Hivi vyuo ndo vinabeba vijana wengi wa mtaani na kuwasaidia kupata kazi na nchini vipo vingi sana....ilikuwa bora serikali kuvipa muda wa kufanya maboresho na sio kuvifungu....
 
kuna haja ya kuvikagua vyuo vyote vilivyo sajiliwa chini ya nacte kama bado vinasifa ya kuendelea kutoa mafunzo.
Japo Vinasaidi sana kuwapa ajira vijana kwa kuwapatia fani mbalimbali lkn vinapaswa kuangaliwa kwa makini ili tusije tukazalisha wataalam feki.
 
mimi nilijua vyuo vikuu, kama vya staili iyo vya kufuta sio ivyo10 vipo vingi sn ambavyo havina hadhi wala vigezo vya kutoa certificate wala dip, wazidi kufatilia kwa makini.
 
Back
Top Bottom