Serikali yahamisha kodi ya simu

Serikali yahamisha kodi ya simu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
KWA UFUPI

  • Hata hivyo, kodi hiyo imerejeshwa kwa staili nyingine baada ya kuongezwa katika tozo la kodi ya manunuzi iliyokuwepo kutoka asilimia 14.5 ya awali hadi asilimia 17.


Dodoma. Serikali imeondoa kodi ya kadi za simu iliyopitishwa na wabunge katika Mkutano wa 13 wa Bunge ambayo ililalamikiwa na wadau na watumiaji wa simu nchini.

Hata hivyo, kodi hiyo imerejeshwa kwa staili nyingine baada ya kuongezwa katika tozo la kodi ya manunuzi iliyokuwepo kutoka asilimia 14.5 ya awali hadi asilimia 17.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salumu, bungeni jana wakati akisoma Muswada wa Sheria ya Manunuzi wa mwaka 2013, ambao uliingizwa bungeni kwa hati ya dharura.

Muswada huo ulipelekwa bungeni kwa hati ya dharura baada ya Rais Jakaya Kikwete kuridhia upitishwe na Bunge kabla ya kuwa sheria kutokana na malalamiko yaliyokuwa yametanda kila kona.

Katika muswada huo ambao ulichukua muda mfupi na kuchangiwa na wabunge wachache, Serikali imesema kuwa kilio cha Watanzania kilisikika na Serikali haikuona haja ya kuendelea na kodi hiyo, badala yake ikaamua kutafuta njia nyingine.

“Mheshimiwa Spika, Serikali imeamua kutafuta njia nyingine ya kukusanya mapato hayo ambayo yalilengwa kupatikana kwa zaidi ya Sh170 bilioni ambayo yangepelekwa katika huduma za umeme na maji, hata hivyo tumepata njia mbadala,” alisema Mkuya.

Alitaja njia hiyo ni kukusanya katika mitandao ya kimawasiliano yote ambayo awali hawakuwa wameilenga na kwamba kupitia njia hizo, wanaweza kupata kiasi cha Sh140 bilioni huku kiasi cha Sh30 zikitarajia kutolewa na kampuni za mawasiliano.

Katika maelezo yake, alisema kuwa kampuni za simu nchini yalikubali kutoa kiasi cha Sh30 bilioni ili kuisaidia Serikali katika kufidia pengo ambalo lingepatikana kwani tayari bajeti ilishapangwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge, Andrew Chenge alisema kuwa Kamati ilikutana juzi mjini Dodoma kwa dharura na kukubaliana jinsi ya kurekebisha kodi na kutafuta njia nyingine ambayo ni kutoza kuongeza kodi katika manunuzi.

Kwa upande wake msemaji wa Kambi ya Upinzani kaika Wizara hiyo Christina Lissu, alilaumu mpango huo kwa madai kuwa hakuna kitu kilichoondolewa na badala yake kilichofanyika ni kiinimacho kwa Watanzania.chanzo.Serikali yahamisha kodi ya simu - Kitaifa - mwananchi.co.tz






 
Jk ni rais wa hovyo kabisa nchi hii imewahi kuwa naye..actually sio nchi hii tu bali africa nzima haijawahi kushuhudia rais wa namna hii
 
mambo yale yale kufuta kodi ya kichwa na kuleta kodi kandamizi ya VAT.
 
Mzigo umeongezwa sana! Hizo 2.5% za kodi zilizoongezwa zitatuliza wengi. Nasikitika kwa kuwa, kama nitapiga bla bla kwa simu, ndio nitalizwa zaidi. Naweka bajeti ya simu, na kuitekeleza kwa nguvu zote.
 
wanashindwa nini kuzibana kampuni za simu kulipa kodi stahiki ukiachilia mbali makampuni ya madini na ukwepaji mkubwa wa kodi.
Lakini sishangai kama mapendekezo haya yanatoka kwa mtu kama chenge
 
Back
Top Bottom