Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema Serikali imetoa maelekezo kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kufuatilia Wafanyabiashara wanaouza vocha za kukwangua kinyume na bei elekezi.
Amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge Tunza Malapo aliyehoji suala hilo, pia JamiiForums.com Wadau kadhaa wakiwemo kutoka Kagera na Songwe (Mji wa Mlowo, Mbozi) walidai kuna changamoto hiyo ambayo imekuwa kero kwa Wanunuaji wakidai Vocha ya Tsh. 500 inauzwa Tsh. 600 au ya Tsh. 1,000 inauzwa Tsh. 1,200.
Pia soma