Kwa taarifa za uhakika hao RITES hizo hisa 51 hawakulipa chochote,badala yake wakatumia rasilimali za TRL kwenda kuomba mkopo wa Dola Mil 100 toka World Bank ili kuendesha TRL.Sasa kwa umbumbumbu wa Serikali yetu watataka kujadiliana nao ili eti wazinunue hizo hisa asilimia 51 za RITES.
Majadiliano ya nini wakati RITES hajaweka chochote zaidi ya kukopa World Bank.Rasilimali ni za Tanzania,TRL ni ya Tanzania mkopo ni wa kampuni ya Tanzania.RITES waanze tuu watuachie TRL yetu na hatutaki wawekezaji toka nje hisa wauziwe watanzania wenyewe wenye uchungu na nchi yao.