Serikali yaiomba Mahakama iruhusu Akaunti ya X na Vifaa vya 'Boni Yai' viingiliwe kwa upekuzi

Serikali yaiomba Mahakama iruhusu Akaunti ya X na Vifaa vya 'Boni Yai' viingiliwe kwa upekuzi

Gemini AI

Member
Joined
May 8, 2024
Posts
91
Reaction score
265
Aiyekuwa meya wa Ubungo, Boniface Jacob, maarufu Boni Yai amesomewa mashtaka mawili ya kuchapisha taarifa za uwongo kwenye mtandao wake wa X (zamani Twitter), ambayo ameyakana.

Serikali imewasilisha maombi mawili, kwanza mahakama imuamuru aruhusu vifaa vyake vya kielektroniki pamoja na akaunti yake ya X ili mpelelezi aweze kuviingilia na kuvifanyia uchunguzi.

Pia, wameomba Mahakama izuie dhamana yake kwa muda. Sasa Mahakama inasikiliza maombi hayo na mawakili wa Serikali wanatoa hoja kufafanua msingi wa maombi hayo, kabla ya mawakili wa utetezi kuyajibu.

Boni Yai amepandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jioni ya leo Alhamisi, Septemba 19, 2024.

Jopo la waendesha mashtaka mawakili wa Serikali wanaongozwa na Job Mrema pamoja na jopo la mawakili wa Jacob linaloongozwa na Peter Kibatala.

MWANANCHI
 
Boni atakuwa kawagomea polisi

Chenga hiyo ,kwamba nitatolea mahakamani ,hilo mosi

Boni alisema kwamba kumteka kwake itakuwa tofauti na utekaji mwingine na pia amegoma kila kitu hadi kutoa maelezo hapo safi....Kutaka kujua source ya habari -source anakuwa undisclosed...Sheria za whistleblowing...wamshitaki kwa hizo taarifa alizochapisha X tu.
 
Mahakama: Tunataka kuchunguza Account yako ya X.

Me: Nimesahau password ya iPhone yangu.
Wakati umeisahau unapigwa kwanza wiki mbili mahabusu bila dhamana wakati taratibu zingine zinaendelea, ukirudi baada ya wiki mbili kesi inahairishwa tena wiki mbili zingine bila dhamana unarudi chini ya uangalizi wa bwana jela
 
Back
Top Bottom