Serikali yaipa Ndege Simba kuipeleka Morocco kwa Fainali ya CAF

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Palamagamba Kabudi akiwa Bungeni Jijini Dodoma leo May 08,2025 kwa niaba ya Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza rasmi kwamba Serikali itawapa Simba SC ndege kuelekea Morocco kwenye mchezo wa fainali.

“Baada ya mafanikio makubwa ya Simba na sasa inaingia kwenye mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho linaloandaliwa na CAF, Simba inakwenda Morocco kupambana na RS Berkane na Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dr Samia imefanya maamuzi ya kutoa ndege itakayoipeleka Klabu ya Simba Morocco kwa ajili ya mchezo huo”

Maamuzi hayo yamefanyika kama sehemu ya jitihada za Serikali za kuipunguzia Simba umbali wa safari na uchovu, Simba SC kwenda Morocco kwa ndege ya abiria kungewafanya wazunguuke na kutumia muda mwingi njiani kutokana na kulazimika kupita nchi tofautitofauti kwa ajili ya kuunganisha ndege.

Hii sio mara ya kwanza kwa Rais Samia kuzisaidia timu za Tanzania Kimataifa (Simba na Yanga) ili kuhakikisha zinafanya vizuri, kwani hata baada ya Yanga kufuzu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika June 3 2023 dhidi ya USM Alger alitoa ndege iliyoipeleka timu Algeria na kuirudisha Dar es salaam.

1746703651191.png
 
RS Berkane, msituangushe mashabiki wenu! Pigeni goli za kutosha kiasi kwamba hata akichezesha Tatu Malogo, Japhet Smart au Kepha Kayombo; Mbereko Fc washindwe kuchomoa.
 
Naomba kuuliza ndg zangu, hivi maafisa wa serikali wakitaja tu serikali bila kuongeza neno inayoongozwa na rais Samia ni kosa kisheria? Maana ni wazi serikali inaongozwa na Dr Samia hakuna kiongozi mwingine, sasa ni kwa nini atajwe tajwe raisi?
 
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Palamagamba Kabudi akiwa Bungeni Jijini Dodoma leo May 08,2025 kwa niaba ya Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametangaza rasmi kwamba Serikali itawapa Simba SC ndege kuelekea Morocco kwenye mchezo wa fainali.

“Baada ya mafanikio makubwa ya Simba na sasa inaingia kwenye mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho linaloandaliwa na CAF, Simba inakwenda Morocco kupambana na RS Berkane na Serikali ya Tanzania inayoongozwa na Rais Dr Samia imefanya maamuzi ya kutoa ndege itakayoipeleka Klabu ya Simba Morocco kwa ajili ya mchezo huo”

Maamuzi hayo yamefanyika kama sehemu ya jitihada za Serikali za kuipunguzia Simba umbali wa safari na uchovu, Simba SC kwenda Morocco kwa ndege ya abiria kungewafanya wazunguuke na kutumia muda mwingi njiani kutokana na kulazimika kupita nchi tofautitofauti kwa ajili ya kuunganisha ndege.

Hii sio mara ya kwanza kwa Rais Samia kuzisaidia timu za Tanzania Kimataifa (Simba na Yanga) ili kuhakikisha zinafanya vizuri, kwani hata baada ya Yanga kufuzu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika June 3 2023 dhidi ya USM Alger alitoa ndege iliyoipeleka timu Algeria na kuirudisha Dar es salaam.
Mimi ni simba ila hata afanye nini, huyu Raisi simpendi hata kidogo
 
Back
Top Bottom