Dar es Salaam. Serikali imeanzisha mfumo mpya wa udahili kwa wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza, kwa kuwalipia ada watakaojiunga na shule binafsi.
Vilevile, imeanzisha utaratibu utakaoshirikisha shule binafsi na zinazoendeshwa na Serikali katika kuteua wanafunzi watakaojiunga na sekondari.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, alisema kuwa utaratibu huo unatarajiwa kuanza kutumika pia kwa wanafunzi wanaotarajiwa kuingia kidato cha tano mwaka huu.
Alisema kuwa mfumo huo utasaidia kuwezesha wahitimu wengi, waliofanya vizuri kupata nafasi za kuendelea na masomo huku pia shule nyingi zikiwa na uhakika wa kupokea wanafunzi.
DarNewsLINE