Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa amesema kuwa baadhi ya akaunti za mitandao ya kijamii za taasisi za Serikali zilidukuliwa kutokana na udhaifu wa taratibu za kiusalama katika usimamizi wa akaunti hizo.
Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo Jumatano Mei 21, 2025, Waziri Silaa ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Makete, Festo Sanga, aliyekuwa akitaka kujua hatua za Serikali kuhusu kusuasua kwa huduma za mawasiliano na kudukuliwa kwa akaunti za mitandao ya kijamii.
"Siku ya jana baadhi ya kurasa za taasisi za Serikali zilipata kuingiliwa. Akaunti hizo tayari zimesharejeshwa, na ni wazi kuwa kulikuwa na changamoto katika taratibu za kiusalama za akaunti hizo ambazo zilipelekea hali hiyo kutokea," amesema Waziri Silaa.
Aidha, katika hatua nyingine, Silaa amesema Tanzania iko mbioni kurusha satellite yake, hatua itakayosaidia kuimarisha huduma za mawasiliano.