Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Edwin Mhede, ameongoza zoezi la utambuzi na uchanjaji wa mifugo mkoani Njombe, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo kwa Mifugo iliyoanzishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, alipokuwa mkoani Simiyu hivi karibuni
Akizungumza na wananchi na wataalam wa mifugo Dkt. Mhede amesema kuwa Serikali kupitia wizara yake imejipanga kuhakikisha mifugo yote nchini inapatiwa chanjo dhidi ya magonjwa hatarishi na kuhakikisha kuwa kila chanjo iliyokusudiwa imewasili na kusambazwa kulingana na mahitaji
"Tunachanja mifugo kwa maana ya ng’ombe dhidi ya homa ya mapafu na tunachanja kuku dhidi ya magonjwa ya kideri, mafua na ndui vilevile tumefika na kuthibitisha kuwa chanjo zote zimefika, na wataalamu waliopatiwa mafunzo wapo kazini kwa ari kubwa wakizingatia miongozo ya wizara "
“Serikali imechukua jukumu kubwa la kugharamia chanjo hizo pamoja na kuwezesha wataalamu wa mifugo, jambo ambalo ninyi wafugaji mmelipongeza. Nimefurahi mmeonesha ari kubwa na kupongeza hatua ya serikali kwa kuwashika mkono kwa zaidi ya asilimia 50 kupitia uwezeshaji wa kitaalamu na chanjo,” alisema Dkt. Mhede
Dkt. Mhede, ameongeza kuwa kupitia zoezi hilo Serikali imepata nafasi kujifunza changamoto za moja kwa moja kutoka kwa wafugaji, zikiwemo masuala ya soko la bidhaa za mifugo. Ameahidi kukaa na pamoja na wadau kuona namna ya kuongeza thamani ya mazao kwa kujenga viwanda vya kusindika maziwa na kuimarisha upatikanaji wa masoko ndani na nje ya Njombe
Chanzo: ITV DIGITAL