Serikali yajizatiti kubidhaisha Kiswahili Kimataifa

Serikali yajizatiti kubidhaisha Kiswahili Kimataifa

University of Dodoma (UDOM)

Public Institution
Joined
Feb 24, 2024
Posts
50
Reaction score
55
Serikali imewahimiza wataalamu wa lugha ya Kiswahili kutumia kikamilifu fursa zinazotokana na ukuaji wa lugha ya Kiswahili duniani, ikiwa ni pamoja na tafsiri, ukalimani, uandishi wa vitabu na utangazaji kwa Kiswahili, katika jitihada za kuibadilisha lugha hiyo kuwa rasilimali ya kiuchumi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 16 la Chama cha Wanafunzi na Wahitimu wa Kiswahili Tanzania (CHAWAKITA) linalofanyika katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuanzia Aprili 8 hadi 9, 2026, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Riziki Pembe Juma, alisema Kiswahili kimeendelea kupata hadhi ya kimataifa, hatua inayofungua milango mipya ya ajira na ubunifu kwa wataalamu wake.

“ Tumieni siku hizi mbili kufanya uchambuzi wa kina, namna mnavyoweza kuibua na kuzitumia fursa zilizopo, na mbinu zinazoweza kutumia kuendelea kuikuza lugha ya kiswahili kimataifa” alisisitiza

IMG_2245.jpeg

Alieleza kuwa ongezeko la matumizi ya Kiswahili katika majukwaa ya kimataifa limechochewa na uamuzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kukitambua Kiswahili kama moja ya lugha zinazotumika katika mikutano yake mikuu, sambamba na kutangaza Julai 7 kuwa Siku ya Kiswahili Duniani.

Kwa upande wake, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri Elekezi, Prof. Razack Lokina, alisema kuwa kongamano hilo linafanyika katika kipindi ambacho dunia inapitia mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia, hivyo kuna umuhimu wa kujadili nafasi ya Kiswahili katika mazingira hayo mapya.

“ Kama wana Taaluma, mna nafasi na kwa da mpana wa kufanya utafiti utakaoisaidia Serikali kubaini fursa zilizopo kwasasa kwenye ulimwengu wa kidigitali” alisema

IMG_2246.jpeg

Alisisitiza kuwa wadau wanapaswa kuangazia namna ya kukiendeleza Kiswahili katika mifumo ya kidijitali, ikiwemo matumizi ya akili unde (Ai), ili kuhakikisha lugha hiyo inaendelea kuwa chombo muhimu cha mawasiliano na maarifa katika karne ya sasa.

Kongamano hilo limewakutanisha washiriki mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, wakiwemo wahitimu wa Vyuo Vikuu na Wanafunzi wanaosoma Vyuo Vikuu na vya Kati kujadili mikakati ya kukuza, kuendeleza na kubidhaisha Kiswahili katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.
 
Back
Top Bottom