Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Komred Kheri James mapema leo, amewasilisha salamu za pole na misaada mbalimbali iliotolewa na Serikali kwa ajili ya Wananchi walio athirika na mvua ya upepo katika Kata ya Mlenge na Itunundu zilizopo katika jimbo la Isimani.
Akizungumza katika zoezi la ugawaji wa vifaa hivyo kwa Wananchi, Komred Kheri James ameeleza kuwa Wananchi 24 wameathirika na mvua hizo za upepo, Wananchi watatu wamefariki dunia na Wananchi 59 hawana makazi kabisa.
Komred Kheri James amewapa pole Wananchi wote waliokumbwa na Changamoto hiyo na amewasilisha salamu za Pole za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassa, pamoja na kukabidhi Chakula, Vifaa vya Ujenzi na mahitaji mengine ya msingi yatakayo weza kuwasaidia katika kipindi hiki kigumu.
Pamoja na mambo mengine Komred Kheri James amewapongeza Wananchi kwa ushirikiano walioutoa kipindi chote cha uokoaji, tathimini na ushirikiano walio utoa kwa kamati ya maafa ya wilaya na Taifa katika kipindi chote cha Changamoto.
Aidha Mheshimiwa Mkuu wa wilaya ameishukuru Ofisi ya Waziri Mkuu, Kamati ya maafa ya wilaya na Kamati ya usalama kwa uwajibikaji wa haraka ambao umerahisisha zoezi la kuwasaidia Wananchi katika changamoto hiyo.
Zoezi la ugawaji wa chakula na vifaa limefanyika katika Kata zote za Mlenge na Itunundu, na kila Mwananchi aliestahili kusaidiwa amekabidhiwa vifaa vyake.