Serikali yakamilisha mchakato wa kuwapa ajira Watumishi 149 wa JKCI Dar Group

Serikali yakamilisha mchakato wa kuwapa ajira Watumishi 149 wa JKCI Dar Group

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dar Group wamepata ajira Serikalini baada ya mchakato kuchukua miaka kadhaa kabla ya kukamilika ambapo leo tarehe 10 Septemba 2025, wamepatiwa mafunzo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo kuhusu utendaji wao Serikalini.

Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya JKCI Dar Group, Idd Lemmah akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dkt. Peter ******* katika mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo, amesema jumla ya waliopata ajira ni 149.

Lemmah amesema Serikali iliichukua Hospitali ya Dar Group na kuikabidhi kwa JKCI ambapo makabidhiano hayo yalihusisha majengo, madeni pamoja na Watumishi, ambapo awali ilikuwa sekta binafsi.

Ameeleza baada ya jitihada mbalimbali kwa kuwasiliana na Wizara ya Utumishi hatimaye mchakato umekamilika na leo tumeanza mafunzo ya kuwasaidia wakati wa utumishi wao wa Umma ambapo tumeanza na mafunzo ya rushwa yaliyoratibiwa na TAKUKURU.

Amesema “Lengo kubwa ni kuhakikisha baada ya kuhamishiwa kwenye utumishi wa umma, wazingatie maadili, kutoa huduma kwa kuzingatia weledi, pia Serikali itaendelea kuwapatia mafunzo mbalimbali kwa lengo la kuwafanya watende wajibu wao inavyotakiwa.



Emmanuel Mapula, Mtumishi wa Hospitali ya JKCI Dar Group.
​
Pia soma: Hospitali ya JKCI-Dar Group mnaihujumu Serikali kwa Kukiuka makubaliano ya Serikali na wafanyakazi mliowakuta
 
Back
Top Bottom