Serikali yakamilisha ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa Bilioni 31.3

Serikali yakamilisha ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa Bilioni 31.3

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Haya wakulugwa uwanja wa Mkapa umeipiga serikali pesa zote hizo ila bado aonekani kama umefanyiwa ukarabati wa bei hiyo.

Hatujapigwa kweli na wajanja wa mjini waliko kwenye mifumo?
=================

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekamilisha ukarabati mkubwa wa Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Temeke, Dar es Salaam kwa gharama ya Shilingi 31,329,180,963.16.

Awamu ya kwanza ya mradi huu iligharimu Shilingi Bilioni 7.44, na baadaye ukarabati ulimaliziwa kwa lengo la kuandaa miundombinu kwa ajili ya mashindano ya CHAN 2025 na AFCON 2027.

Uwanja huu wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 60,000 umewezesha ajira mbalimbali ikiwemo:

  • Ajira za muda 1,200 kwa mafundi, wahandisi, wasimamizi na wahudumu wa usalama wakati wa ukarabati.
  • Ajira za kudumu takribani 150 kwa usimamizi wa uwanja, matengenezo, usafi na huduma za kiufundi baada ya ukarabati.
 
hawa jamaa wanakula haswaa.
 
We're fucked up
20250912_153553.jpg
 
Mambo ya kijinga sana na hauwezi kumsikia Samia wala kikaragosi yeyote akikemea huu ufisadi, ile ni pitch ya bilioni 31 kweli??
 
Back
Top Bottom