Serikali yakataza wafugaji kuweka alama kwenye ngozi za mifugo, hasa ng’ombe

Serikali yakataza wafugaji kuweka alama kwenye ngozi za mifugo, hasa ng’ombe

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
1575454417227.png

Serikali imewakataza wafugaji kuweka alama kwenye ngozi za mifugo yao hasa ng’ombe kwani kufanya hivyo kunashusha thamani ya ngozi za Tanzania, na badala yake imewataka waweke alama za hereni kwenye masikio ya mifugo yao ili kulinda ubora wa ngozi za mifugo yao.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa Machinjio ya Vingunguti ambaopo alibainisha kuwa alama hizo kwenye ngozi za mifugo zinafanya thamani ya ngozi kutoka nchini kuwa chini.

Amesema Serikali tayari imekwishampata mwekezaji kutoka Misri ambaye amekubali kuwekeza kwenye kiwanda cha ngozi cha Mwanza hatua ambayo italihakikishia Taifa soko la ngozi.

Kuhusu ujenzi wa machinjio hiyo Waziri Mkuu amemtaka mkandarasi ahakikishe kwamba anakamilisha ujenzi huo mwishoni mwa mwezi huu kama alivyoamriwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Amesema amefurahishwa na hatua ya mkandarasi huyo ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ya kuongeza idadi ya watalaam na mafundi ili kuhakikisha kwamba kazi hiyo inafanyika haraka na kukamilika kwa wakati ulioamriwa na Rais Magufuli yaani Desemba 30, mwaka huu.

Waziri Mkuu Majaliwa amemtaka Mshauri Mwelekezi wa mradi huo ambaye ni M/SCONS AFRIKA LIMITED na FB Consultant wa Dar es Salaam asimamamie kwa karibu ili kujiridhisha kuwa maelekezo yote yaliyopo kwenye michoro ya ujenzi huo yanazingatiwa na mkandarasi.

Amesema Serikali imeamua kujenga machinjio hayo ya kisasa ya Vingunguti baada ya kugundua kwamba wafanyabiashara wa mifugo na mazao yake katika machinjio hayo, walikuwa wakifanya kazi zao kwenye mazingira duni na kwamba nyama iliyokuwa ikitoka kwenye machinjio hayo ilikuwa haikubaliki kwenye soko la nje ya nchi.

“Uamuazi wa Serikali kujenga machinjio haya, utaifanya nyama inayotoka hapa ikubalike kwenye masoko ya nje ya nchi, hatua ambayo itaongeza mzunguko wa fedha kwenye eneo hili wakati Serikali na Manispaa watanufaika kwani kutakuwa na ongezeko la makusanyo ya kodi,” aliongeza Mheshimiwa Majaliwa.


Chanzo: Swahili Times
 
Kazi ya kuweka Alama ilifanywa na serikali na tulikupa 500 kwa kila Ng’ombe
 
Hivi anajua kuwa siku hizi ngozi hazina thamani tena na zinatupwa tu
Na Soko hilo wameliuwa wao?
 
Mh, yaani umpige chapa umtoe alama hivyo? Hao ni viumbe hai jamani, wanahisi maumivu kama sisi
 
Hapo ndipo unafika unajiuliza hawa wanaojidai watetezi wa haki za wanyama hawali nyama?
Kuchinjwa ni kitu cha one time na kinakuwa cha muda mfupi, sasa kuuachia majeraha yanayomuumiza kwa muda mrefu ni mateso zaidi
 
Lakini ng'ombe haishi milele maana anafugwa ili achinjwe...

Huoni kama kumchinja ni ukatili zaidi?
Kwa hiyo kama ng'ombe au mbuzi tunawachinja hata tukiwatoa utumbo kisha tukawaacha ni sawa?
 
Ng'ombe wa maziwa Kenya hata kuchapwa fimbo ni marufuku wanasema watapata stress na kupunguza uzalishaji wa maziwa,sijui akipigwa Chapa kama hio atakua na hali gani.
 
Ng'ombe wa maziwa Kenya hata kuchapwa fimbo ni marufuku wanasema watapata stress na kupunguza uzalishaji wa maziwa,sijui akipigwa Chapa kama hio atakua na hali gani.

Umenikumbusha kuna siku nilikuwa napita sehemu nikamuona jamaa anamchapa sana punda ambae alikuwa amembea mzigo mzito sana
Sidhani kama atanisahau yule jamaa
Nilimkaripia sana sana
Na baada ya hapo nikampa fundisho na kumuuliza kama huyo punda ndio tegemeo lake katika maisha ya kila siku na kumuungizia riziki
Yaani jamaa mpaka machozi yalimlenga
Nikamwambia siku nyingine mkatie majani na uwe na maji pia kama unatembea masafa marefu hivi
Kutesa wanyama sipendi kabisa
 
Back
Top Bottom