Serikali yakemea watumishi wa umma wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja

Fuatilieni uchaguzi achaneni na mambo ya ajabu ajabu yasiyo na maslahi ya umma
 
Attachments

  • Screenshot_2024-07-16-21-00-20-1.png
    Screenshot_2024-07-16-21-00-20-1.png
    420.8 KB · Views: 3
Ukiona serikali haiwezi kudeal na matatizo ya kiuchumi na kijamii yanayoaffect mtu mmoja mmoja na nchi nzima as a whole...afu inataka ideal na watu wanafanya nini chumbani kwao usiku.. ujue tuna safari ndefu sana kama taifa
Akili yao ndipo imegota hapo! Hakuna degree, Masters, PhD wala nini! Copy and paste tu hapo!
 
Ukiona serikali haiwezi kudeal na matatizo ya kiuchumi na kijamii yanayoaffect mtu mmoja mmoja na nchi nzima as a whole...afu inataka ideal na watu wanafanya nini chumbani kwao usiku.. ujue tuna safari ndefu sana kama taifa
Ni muhimu pia viongozi wetu watufafanulie maadili ya mtanzania ni yepi. Hatusikii viongozi wetu wakikemea (kutoka moyoni) ubadhirifu na wizi wa mali ya umma, wizi wa kura, rushwa, uvunjifu wa haki za binadamu nk kama ni ukiukaji wa maadili ya Mtanzania. Hebu angalia kinachaendelea kwenue unadikishaji kwenye daftari la wakaazi.
 
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Xavier Daudi, amekemea vikali vitendo vya uhusiano ya jinsia moja miongoni mwa watumishi wa umma, akisisitiza kuwa vitendo hivyo ni kinyume na maadili, mila, na desturi za Kitanzania.

Daudi ametoa kauli hiyo, Alhamisi Oktoba 17, 2024, Jijini Dodoma wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kati ya taasisi zinazohusika na usimamizi wa maadili.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Daudi ameeleza kuwa ofisi yake imeanza kupokea malalamiko kuhusu mmomonyoko wa maadili, hususan vitendo vinavyohusiana na uhusiano ya jinsi moja, jambo ambalo limepingwa vikali na serikali.

"Vitendo hivi vinakiuka maadili ya Kitanzania, na tunapaswa kukumbuka kuwa si kila kitu kinachotoka nje ya nchi ni kizuri," amesema Daudi, akiongeza kuwa vitendo hivyo vinaharibu utaratibu wa maadili kazini.

Daudi amebainisha kuwa serikali tayari imeanza kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaojihusisha na vitendo hivyo, na amesisitiza kuwa kuwahamisha watumishi hao hakutatui tatizo, kwani wanaweza kuendeleza tabia hizo katika maeneo mapya.

"Tulikemee hili kwa nguvu zote. Hatuhitaji mambo kama hayo serikalini. Sisi ni taifa lenye maadili yetu, na hili si sehemu ya maadili hayo," ameongeza Daudi.

Daudi pia ametoa wito kwa viongozi wa dini na jamii kuchukua hatua kali dhidi ya vitendo vya mahusiano ya jinsia moja, akisisitiza umuhimu wa kulinda maadili ya taifa na kuhakikisha jamii inaendelea kuzaliana kwa mujibu wa mila na desturi za Kitanzania.

Alisema, "Tufikirie mara mbili; wananchi wameacha kuzaliana, na tukiendelea hivi, baada ya miaka kadhaa tutashuhudia wanaume na wanawake wakiingia kwenye ndoa za jinsia moja. Ni lazima kila mmoja achukue nafasi yake, hasa taasisi za dini."

Chanzo: Jambo Tv

SERIKALI YAKEMEA WATUMISHI WA UMMA WASIOFUATA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA

NA. LUSUNGU HELELA-DODOMA

SERIKALI imeonya ukiukwaji wa maadili kwa watumishi wa umma ikiwa ni pamoja na viashiria vya mapenzi ya jinsia moja na mavazi yasiyofaa jambo ambalo limekuwa likichafua taswira ya serikali.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 17,2024 jijini Dodoma Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi,wakati akifungua kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora baina ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka simamizi za maadili ya kitaluma.

Bw.Daudi amesema kuwa Ofisi imeanza kupokea tuhuma na malalamiko kuhusu kuwepo kwa viashiria vya mmomonyoko wa Maadili kinyume na mila na desturi za nchi yetu vinavyohusu vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kwa baadhi ya watumishi wa umma.

Amesema kuwa, vitendo hivyo ni miongoni mwa vitendo vya kijinai kwa mujibu wa sheria za nchi lakini pia ni vitendo vya kinyume na maadili kwa mujibu wa miongozo ya utumishi wa umma.

“Hivyo, tumieni kikao kazi hiki, kujadili na kubadilishana uzoefu ili kuja na mapendekezo ya namna sahihi ya kudhibiti vitendo hivi na namna sahihi ya kushughulikia masuala haya yatakapojitokeza katika maeneo yenu ya kazi kwa baadhi ya watumishi wanaohusishwa navyo ili kuepuka kuchafua taswira ya utumishi wa umma kwa ujumla,”amesema Bw.Daudi

Aidha ameziomba taasisi za Dini nchini kusimamia maadili na kuonya na kukemea vitendo hivyo vya ndoa ya jinsia moja katika jamii ya kitanzania mana wao wana nguvu na Sauti kubwa ya kusikika zaidi.

“Hivi sasa zipo nchi zimeacha kuzaliana kutokana na kushamiri kwa vitendo hivyo vya mapenzi ya jinsia moja,,Tanzania hatutaki kufika huko ndio mana tunakemea,”amesema

Kuhusu mavazi yasiofaa ameelekeza watumie waraka namba 6 wa utumishi wa umma unaozungumzia mavazi kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaochafua taswira ya serikali kwa kuvaa hovyo ndani na nje ya utumishi.

Amesema kuwa zipo taasisi ambazo viongozi wake wameanza kulegalega kwa kutochukua hatua na kuacha watumishi wakivaa mavazi kinyume cha maadili ya utumishi wa umma.
Safi sana!
Inahitajika misimamo kama hii.
 
Ni muhimu pia viongozi wetu watufafanulie maadili ya mtanzania ni yepi. Hatusikii viongozi wetu wakikemea (kutoka moyoni) ubadhirifu na wizi wa mali ya umma, wizi wa kura, rushwa, uvunjifu wa haki za binadamu nk kama ni ukiukaji wa maadili ya Mtanzania. Hebu angalia kinachaendelea kwenue unadikishaji kwenye daftari la wakaazi.
Si ndo hapo....hayo maadili yashakuwa chaka la kucensor watu
 
Achen makasiriko na unafiki, hamjawahi kula kiboga jaman? Tufanye mambo ya msingi mapenzi ni faragha ya mtu tusiingiliane kwa kweli
 
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Xavier Daudi, amekemea vikali vitendo vya uhusiano ya jinsia moja miongoni mwa watumishi wa umma, akisisitiza kuwa vitendo hivyo ni kinyume na maadili, mila, na desturi za Kitanzania.

Daudi ametoa kauli hiyo, Alhamisi Oktoba 17, 2024, Jijini Dodoma wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora kati ya taasisi zinazohusika na usimamizi wa maadili.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Daudi ameeleza kuwa ofisi yake imeanza kupokea malalamiko kuhusu mmomonyoko wa maadili, hususan vitendo vinavyohusiana na uhusiano ya jinsi moja, jambo ambalo limepingwa vikali na serikali.

"Vitendo hivi vinakiuka maadili ya Kitanzania, na tunapaswa kukumbuka kuwa si kila kitu kinachotoka nje ya nchi ni kizuri," amesema Daudi, akiongeza kuwa vitendo hivyo vinaharibu utaratibu wa maadili kazini.

Daudi amebainisha kuwa serikali tayari imeanza kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaojihusisha na vitendo hivyo, na amesisitiza kuwa kuwahamisha watumishi hao hakutatui tatizo, kwani wanaweza kuendeleza tabia hizo katika maeneo mapya.

"Tulikemee hili kwa nguvu zote. Hatuhitaji mambo kama hayo serikalini. Sisi ni taifa lenye maadili yetu, na hili si sehemu ya maadili hayo," ameongeza Daudi.

Daudi pia ametoa wito kwa viongozi wa dini na jamii kuchukua hatua kali dhidi ya vitendo vya mahusiano ya jinsia moja, akisisitiza umuhimu wa kulinda maadili ya taifa na kuhakikisha jamii inaendelea kuzaliana kwa mujibu wa mila na desturi za Kitanzania.

Alisema, "Tufikirie mara mbili; wananchi wameacha kuzaliana, na tukiendelea hivi, baada ya miaka kadhaa tutashuhudia wanaume na wanawake wakiingia kwenye ndoa za jinsia moja. Ni lazima kila mmoja achukue nafasi yake, hasa taasisi za dini."

Chanzo: Jambo Tv

SERIKALI YAKEMEA WATUMISHI WA UMMA WASIOFUATA MAADILI YA UTUMISHI WA UMMA

NA. LUSUNGU HELELA-DODOMA

SERIKALI imeonya ukiukwaji wa maadili kwa watumishi wa umma ikiwa ni pamoja na viashiria vya mapenzi ya jinsia moja na mavazi yasiyofaa jambo ambalo limekuwa likichafua taswira ya serikali.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 17,2024 jijini Dodoma Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Xavier Daudi,wakati akifungua kikao kazi cha kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya maadili na utawala bora baina ya taasisi simamizi za maadili ya utendaji na mamlaka simamizi za maadili ya kitaluma.

Bw.Daudi amesema kuwa Ofisi imeanza kupokea tuhuma na malalamiko kuhusu kuwepo kwa viashiria vya mmomonyoko wa Maadili kinyume na mila na desturi za nchi yetu vinavyohusu vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kwa baadhi ya watumishi wa umma.

Amesema kuwa, vitendo hivyo ni miongoni mwa vitendo vya kijinai kwa mujibu wa sheria za nchi lakini pia ni vitendo vya kinyume na maadili kwa mujibu wa miongozo ya utumishi wa umma.

“Hivyo, tumieni kikao kazi hiki, kujadili na kubadilishana uzoefu ili kuja na mapendekezo ya namna sahihi ya kudhibiti vitendo hivi na namna sahihi ya kushughulikia masuala haya yatakapojitokeza katika maeneo yenu ya kazi kwa baadhi ya watumishi wanaohusishwa navyo ili kuepuka kuchafua taswira ya utumishi wa umma kwa ujumla,”amesema Bw.Daudi

Aidha ameziomba taasisi za Dini nchini kusimamia maadili na kuonya na kukemea vitendo hivyo vya ndoa ya jinsia moja katika jamii ya kitanzania mana wao wana nguvu na Sauti kubwa ya kusikika zaidi.

“Hivi sasa zipo nchi zimeacha kuzaliana kutokana na kushamiri kwa vitendo hivyo vya mapenzi ya jinsia moja,,Tanzania hatutaki kufika huko ndio mana tunakemea,”amesema

Kuhusu mavazi yasiofaa ameelekeza watumie waraka namba 6 wa utumishi wa umma unaozungumzia mavazi kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaochafua taswira ya serikali kwa kuvaa hovyo ndani na nje ya utumishi.

Amesema kuwa zipo taasisi ambazo viongozi wake wameanza kulegalega kwa kutochukua hatua na kuacha watumishi wakivaa mavazi kinyume cha maadili ya utumishi wa umma.
Sasa serikali isiyokuwa na macho wala masikio imejuaje! Nachoweza kusema aliyelianzisha na kuisingizia serikali naye ni mshiriki bila kushiriki asingelijua hili kama sisi ambavyo hatuwajui huku mitaani tunakoishi nao.
 
Unafiki tuu huko wanafanya hakuna mtu asiyefanya huko ni wachache sanaa so kila mahali kuna watuu sema tu usiri, hata huyo aliyeleta hii issue aseme kama hajawahi kula tigoo hahah
 
MHESHIMIWA Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma

Nikukumbushe:

Utumishi wa Umma na Utawala wa nchii hii hauendi kwa mila na desturi.

Nchi hii inaendeshwa na UTAWALA WA SHERIA

Pamoja na

KANUNI NA MIIKO YA KIMAADILI YA UTUMISHI ILIYOANDIKWA KWENYE MAKARATASI

Na sio Mila na Desturi

Unakwama wapi Katibu Mkuu ???????

Sisitiza sheria, kanuni na maadili ya utumishi YALIYOANDIKWA VITABUNI
 
Anataka aonekane na yeye kasema kituu, anaingilia faragha za watu. Kuna habari za kijinga jamani
 
Back
Top Bottom