Majibu hayo kutoka kwa Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba yamekuja baada Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kuuliza sababu za Serikali kupokea Tsh. Bilioni 700 kutoka BARRICK na kuachana na mashauri 1,097 ya kesi ya madai ya Tsh. Trilioni 360 za usafirishaji Makinikia.
Akijibu swali hilo Dkt. Mwigulu amesema baada ya kuibuka mzozo kati ACACIA na Serikali, kampuni ya ACACIA iliiuzia kesi hizo BARRICK na Rais Magufuli aliunda timu ya kufanya majadiliano mwaka 2018 ambapo makubaliano yaliisha mwaka 2020 na sherehe zilifanyika Ikulu mbele ya Rais Magufuli.
Waziri Mwigulu amesema “Tanzania tukakubali kuachilia Tsh. Trillioni 360 tumalize shauri lile na tukaunda kampuni ya Twiga na nchi nzima tukasherehekea, Kampuni ile ina ubia wa 16% na Serikali ina asilimia 84 kwa Barrick".