Serikali yakiri kuachana na madai ya Tsh. Trilioni 360 za Makinikia

Rubbish
 
Mpina angemuuliza hilo swali Mwendazake na VP aliyekuwa Waziri wa Fedha na Waziri wa Madini na yule kamishna wa TRA aliyeondolewa ndio wanajua kwa nini hawakuzidai hizo pesa badala yake wakachukua bil.700 tuu..
Wewe kizazi chenu ni fungu la hasara
 
Majibu hayo kutoka kwa Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba yamekuja baada Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kuuliza sababu za Serikali kupokea Tsh. Bilioni 700 kutoka BARRICK na kuachana na mashauri 1,097 ya kesi ya madai ya Tsh. Trilioni 360 za usafirishaji Makinikia.

Akijibu swali hilo Dkt. Mwigulu amesema baada ya kuibuka mzozo kati ACACIA na Serikali, kampuni ya ACACIA iliiuzia kesi hizo BARRICK na Rais Magufuli aliunda timu ya kufanya majadiliano mwaka 2018 ambapo makubaliano yaliisha mwaka 2020 na sherehe zilifanyika Ikulu mbele ya Rais Magufuli.

Waziri Mwigulu amesema “Tanzania tukakubali kuachilia Tsh. Trillioni 360 tumalize shauri lile na tukaunda kampuni ya Twiga na nchi nzima tukasherehekea, Kampuni ile ina ubia wa 16% na Serikali ina asilimia 84 kwa Barrick".
 
Sasa kwa nn tulikamata makinikia, kwanini TMAA ilivunjwa, sababu za kukamata zilikuwa ni zipi, na je hizo sababu hazipo tena. Kwanini watumishi wa TMAA walishushwa mishahara
 
Heri nusu shari kuliko shari kamili. Tumepata hicho kiasi kiduchu lakini kuibwa kwa makinikia kumesitishwa na sisi tumepata asilimia 16 ya kampuni mpya. Hiyo ni nzuri sana.
 

Cha kuchekesha biashara, mtaji na kila kitu uchanganye Barrick na ACACIA hawajahi kufikia $192b.
 
Bil.700 ililipwa kwa mikupua 3,tafuta habari zake zipo na walikuwa wanatangaza.
Jibu swali la zilipo trillion 360. Hizi bilioni 700 hazikuwepo kwenye swali la msingi kwani ni jibu tofauti! Kama kweli una jibu zizungumzie kidogo zilipo trillion 369 tukuelewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…