#COVID19 Serikali yakusudia kuchanja asilimia 60 ya Watanzania Chanjo ya Coronavirus

#COVID19 Serikali yakusudia kuchanja asilimia 60 ya Watanzania Chanjo ya Coronavirus

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Dar es Salaam. Baada ya chanjo ya Covid-19 kuwasili nchini Serikali imejiweka lengo la kuwachanja asilimia 60 ya Watanzania wote.
Waziri wa Afya, Dk Doroth Gwajima amesema awamu ya kwanza ya chanzo hiyo itatolewa kwa makundi ya mstari wa mbele ambayo yatawekwa wazi siku ya kesho.

Amesema kwa kuanzia watachanjwa watu walio kwenye mstari wa mbele lakini lengo ni kuwafikia watanzania wote watakaohitaji.

“Serikali ya awamu ya sita imejipanga kuhakikisha kila Mtanzania kwa hiari yake bila malipo atapata chanjo.

“Kuhusu makundi yatakayoanza tutaweka wazi kesho ni akina nani na utaratibu upi utatumika, zitapatikana wapi haya yote tutayaeleza,” amesema Dk Gwajima.

Mwananchi
 
Chanjo ya majaribio ianze kwa mapolisi kwanza wageuke mazombi

Chanjo ya majaribio?? Majaribio ya chanjo hii yalikwisha hata bado hujaambiwa inakuja. Ujinga ndio tatizo kuu la nchi hii. Kama wewe hapa unasambaza taarifa potovu na chuki ndani yake. Haya, tuseme polisi wawe mazombi - wewe au taifa hili litafaidika vipi??

Jielimishe na pata ufahamu wa mambo kabla hujafanya uharibifu kwenye jamii. Acha alama chanya katika dunia hii - ujinga na chuki nenda navyo kaburini.
 
Dar es Salaam. Baada ya chanjo ya Covid-19 kuwasili nchini Serikali imejiweka lengo la kuwachanja asilimia 60 ya Watanzania wote.
Waziri wa Afya, Dk Doroth Gwajima amesema awamu ya kwanza ya chanzo hiyo itatolewa kwa makundi ya mstari wa mbele ambayo yatawekwa wazi siku ya kesho...
Africa kuna vituko sana, toka kelele za chanjo zimeanza waliopata chanjo kamili hawafiki 5% ya waafrika wote barani Africa, lakini kelele za chanjo zinavyopigwa utafikiri hiyo chanjo yenyewe wanapewa nyingi ahahahahaha
 
Hatari tupu
IMG-20210723-WA0066.jpg
 

Attachments

  • IMG-20210723-WA0066.jpg
    IMG-20210723-WA0066.jpg
    62.1 KB · Views: 2
Back
Top Bottom