Serikali yalifungia kanisa la Spirit Word Ministry

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1678709667404.png

Serikali imesitisha huduma za Spirit Word Ministry inayoongozwa na Askofu Dk Ceasar Masisi yenye makao makuu yake Stakishari, Ukonga jijini Dar es Salam.

Taarifa iliyotolewa jana Machi 12 na uongozi wa Sprit Word Ministry kwenye mtandao wa mchungaji huyo, imeeleza kuwa wamepokea maelekezo ya kusitisha huduma kanisani hapo na kwenye matawi yake hadi hapo watakapopokea malekezo mengine.

“Machi 9, 2023 Spirit Word Ministry imepokea notisi ya maelekezo kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, ambapo pamoja na malekezo mengine imeielekeza taasisi ya Spirit Word Ministry kusitisha shughuli zote za uendeshaji wa taasisi mara moja mpaka pale taasisi itakapopewa maelekezo mengine,” imeeleza taarifa hiyo.

Kutokana na zuio hilo, taasisi hiyo imelazimika kutoa taarifa kwa waumini wake ikiwataka kufuata maelekezo waliyoyapokea.

“Kufuatia maelekezo hayo, Spirit Word Ministry inawatangazia watu wote kuwa imesitisha shughuli zake zote ikijumuisha ibada/ ratiba za madarasa ya Jumapili au siku yoyote ile, katika matawi yote ya Spirit Word Ministry.

“Madarasa ya mitandao ya kijamii kama Whatsapp na Telegram, vipindi vilivyokuwa vikiruka kupitia mitandao ya kijamii na TOP TV na shughuli zingine zote ambazo zimekuwa zikiendeshwa na huduma ya Spirit Word Ministry,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kwamba kusitishwa huko kutaendelea mpaka pale taasisi itakapopata maelekezo mengine kutoka kwa mamlaka husika.

MWANANCHI
 
Huyu jamaa alikuwa anauza vipodozi Sasa Kahamia huku!? Daaa
 
View attachment 2548997

Watanyooshwa sana alianza suguye
 
Huyu Dr.Elizabeth Kilele, mke wa askofu husika atakuwa ndiye mjibu mashtaka katika kesi Korti ya Rufaa ya Kenya yenye kichwa "Court of Appeal-Court Application E242 of 2020- 23 Oct. 2020-Kenya
Kenneth Kipkurui Mibei v. Elizabeth Kilele (and others)?
 
Back
Top Bottom