Mtanzania, tuamini tunaoishi Mbeya! RC huyo kaongea na vyombo vya habari mara tatu akisisitiza kuwa hakuna maafa Kyela, ni mafuriko ya kawaida tu! Wewe mwenyewe mpigie Mkuu wa Wilaya, Mashimba H. Mashimba, utaelewa tu kuwa kuna tatizo kubwa mahali fulani. Lazaros
Lazarosmtindi,
Kama kaongea kwenye vyombo vya habari si lete hiyo quote? Mara tatu nzima na bado mnashindwa kuja na hiyo statement hapa, why? Hakuna hata gazeti moja ambalo liliweza kuandika alichosema?
Mimi nimeongea na mkuu wa wilaya na anasema sio kweli na badala yake ni siasa za Kyela. Pia najua mkuu wa mkoa alikuwa Kyela akisaidiana na wengine kusimamia maafa na misaada, sasa hii ya kusema Kyela hakuna maafa inatoka wapi?
Badala ya kuongea maneno toeni misaada na pelekeni Kyela, kama mtazuiwa kwasababu mkuu wa mkoa anakataza, mtakuwa na ushahidi wa kutosha.
Mkuu wa wilaya anapokea misaada, mbunge naye alitoa njia za kufikisha misaada, kama kuna watu wanataka kusaidia Kyela kuna njia na utaratibu wa kufanya hivyo.
Haya mengine ya wapambe wa wanasiasa wanaokuja kuchafuana hapa JF kwa cost ya Kyela, mimi naona ni kupoteza muda. Politics zitarudi 2010, kwasasa chapeni kazi.
Tuache maneno matupu hata mahali ambapo tunaweza kuonyesha kwa vitendo. Wale waliotoa misaada yao Kyela wanajua ilipokelewa bila mizengwe yeyote. Kama kuna mtu alitaka kutoa na akazuiwa labda ndio leteni experiences zenu, vingine hizi politics politics politics kwa cost ya maendeleo ni kupoteza muda.
Hapa kuna waandishi wa habari, si mtafuteni mkuu wa wilaya na kumhoji? Pia kama ni kweli Mwakipesile alisema hivyo, si Mwakyembe aseme wazi kwenye TV au hata gazetini? Maana mtu anayesema hakuna maafa wakati watu wanateseka ni muuaji na lazima aumbuliwe. Kama mbunge ana habari hizo, kwanini akae kimya? Tuwe wakweli, kuna mambo mengine ni black and white na hakuna haja ya kujifanya kuna rangi nyingine katikati. Wenye habari waende kwenye TV na kumsagia mkuu wa mkoa kwa upuzi huo.
Kinachoshangaza, wanalalamika chinichini huku wanajifanya wana ushahidi.
Imefika mahali I am really tired na siasa hizi za ugomvi kila siku kule nyumbani. Njia ya kumuumbua mnafiki ni kusema ukweli. Wenye ukweli muumbueni Mwakipesile waziwazi na sio kueneza uvumi pembeni.
Mkuu wa mkoa naye anajidai yeye ndio katoa misaada mingi wakati kila mtu anajua hiyo misaada ni ya serikali na mingine ya watu ambao walipitishia kwake kwasababu tu ni mkuu wa mkoa.
Siasa za Afrika ni ujinga mtupu, nafikiri kwasababu wananchi tunaendeleza ujinga huo, na wao wanaona ni fair game.