GE2025 Serikali yamwaga bilioni 1.6 kwa wananchi wa Uvinza walioachia eneo la SGR kama fidia

GE2025 Serikali yamwaga bilioni 1.6 kwa wananchi wa Uvinza walioachia eneo la SGR kama fidia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
CCM wanambinu zao za dakika zajioni katika kuzitafuta kura. Lakini kama uchaguzi usikuwepo mwaka huu basi bila shaka wananchi wakeendela kuteseka katika kudai fidia zao
====================

Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) imelipa zaidi ya shilingi bilioni 1.6 kwa wananchi 213 wa Kijiji cha Mpeta, Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma, waliopisha ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Tabora–Kigoma.

Mthamini na msimamizi wa zoezi hilo, Hassan Mbaga, amesema ulipaji huo ni sehemu ya awamu ya pili ya fidia kwa kipande cha sita cha mradi, na kwamba utatekelezwa kwa hatua kadri maeneo yanavyohitajika.

Katibu Tarafa wa Nguruka, Bw. Lyola Proches, aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, amewataka wananchi kutumia fedha hizo kwa busara na maendeleo, akisisitiza umuhimu wa kurejesha miundombinu waliyoipisha.
 
Back
Top Bottom