Serikali yamwaga mashangingi: Hatujifunzi tu kutoka Rwanda jinsi Kagame anavyotawala?


mimi ikifikia hapa huwa nachoka kabisaaaaaaa
 


Lah, ndugu yangu nakushauri usipite tena huko kwenye mitaa ulikopita leo.

Hivi kweli umejiuliza kama kweli makatibu wakuu na wakurugenzi wa idara wanakwenda vijini kuhimiza maendeleo? na ni maendeleo gani hayo wanayohimiza? Na je umejiuliza ni kwa nini barabara za vijijini ni mbovu?
 

ina maana hayo mashangingi 700 ni ya makatibu wakuu na wakurungenzi TU? tena wa wizarani tu? HAkuna watendaji wengine?
 
ina maana hayo mashangingi 700 ni ya makatibu wakuu na wakurungenzi TU? tena wa wizarani tu? HAkuna watendaji wengine?

OK,

Sasa ni jambo lipi la maana; kujenga barabara za vijijini au kununua mashangingi hayo kila baada ya miaka mitatu.


Hata kama kweli kuna ulazima, je ni kweli yalihitajika hayo 700 yote wakati mwaka juzi tu yaliingizwa mengine idadi karibu sawa na hiyo? Kama wangekuwa serious, wangekuwa na utaratibu wa kuwa na magari machache ya aina hiyo kwa ajili ya safari za namna hiyo yakawa yanatumiwa na viongozi wote kwa vile siyo kweli kuwa wote huwa wananaenda huko vijijini kwa pamoja kila siku.
 

Yep yep...nakubaliana na wewe kabisa.
Naona tunamuhitaji Capt Moussa Dadis Camara (leader of Guinea Coup) kutuwekea mambo sawa hapa.Utani na mizaha juu ya maisha ya watanzania vimezidi mno.
 
Naam na Wanyarwanda wanampenda kweli kweli maana wanaona mabadiliko makubwa ndani ya nchi yao. Siyo Mafisadi na waroho wa utajiri wa haraka haraka wanaofisadi Tanzania kila kukicha waliojaa ndani ya chama cha mafisadi na serikali.

Katika hali kama hii,huku Tanzania tukijishangaa tutawakuta wanyarwanda wako kama wachina na si ajabu tukawa na ziara za kwenda kuomba misaada kwao! May U,God The Almighty deal with these Tanzanian Leaders....
 
Priorities ndugu zangu!
Juzi nimeangalia magari ya mawaziri India..yaani ni ya kawaida mno!
Sasa kama viongozi kwao priority ni mashangingi na sii barabara nzuri vijjijini na kila baada ya miaka 5 tunazidi kuwachagua hawa2 je wajinga ni sisi wanainchi au viongozi?
Je wanaweza kuondolewa kwa kura? Tz inawezekana? Na Je change for better or worse? Tuangalie ya Chiluba Zambia!

Hivi kweli Katibu wa Wizara anahitaji VX ya 100m toka Masaki kuja ofsini Posta wakati shule zinafungwa kwa watoto wetu kukosa chakula?
 
Mh, kisha tunaamiwa kasungura kenyewe kadogo! LAiti wananchi wangejua ukweli na udghaifu na ubovu wa viongozi wetu, wasingeikubali serikali hii ya Kagoda Ltd, EPA, Richmonduli na kiwira.
 
Tatizo ni zile 10% za D.T Dobie na International Motors... wenyewe wanaziita "commision" kwa kuwaletea biashara. The higher the deal, the higher the commision.


1. Je, sheria ya manunuzi ilifuatwa? Tenda ya kununua ilitangazwa lini na gazeti gani?
2. Lakini nina wasiwasi na habari hii??? Accounting officer gani serikalini ananunua magari hayo? kwa sababu, kwa taratibu za serikali hainunui magari yote halafu ikagawia wizara na idara zake (Labda yawe ya msaada na huelekezwa kwenye sekta maalumu). Kila wizara (na idara zinazojitegemea e.g. TANROADS) inajitegemea kununua magari yake. Isije ikawa aliyeona kaona magari ya D.T. Dobie na Toyota Motors yanateremshwa bandarini akadhani yote ni ya serikali.
 

Samahani FMES, unanichanganya kidogo. Unazungumzia Warundi au Wanyarwanda? Naona umechanganya Warundi na Kagame!!!!!
 
- Huyu Kagame anatakiwa The Haque kujibu mashitaka ya kuua wananchi wengi sana, amehusika na kuua wananchi laki nane yaani wananchi 800,000 kwa kweli hata awe kiongozi safi lakini binafsi siwezi kumpa credit, mikono yake imejaa damu sana,


...hapana mkuu,hapo naona unachanganya mambo,hao laki nane waliokufa ilikuwa ni kazi ya interahamwe supported by France,Kagame is the one who stopped genocide baada ya kukamata Kigali na kuanza kuwakimbiza Interahamwe(hutu extremist) na for the records kagame hana mashtaka wala hatakiwi The Hague,na yule mama msaidizi wake kishaachiwa na sasa yuko Rwanda inaonekana France hawana kesi ni politics tuu!
 
TANZANIA hatuwezi kwa kutumia internet kutengeneza MAGARI yetu wenyewe?


BAADA ya yote nilikuwa ninajiuliza hivi hatuna mechanical engineers wa kutosha ili tuwaweke mahala pamoja kisha tuwanunulie ama Landrover, Tata au Toyota halafu saloon simple kama Hyundai au Honda na tuwape MTIHANI wa kutengeneza gari la Kitanzania/Kiafrika hapa hapa nchini nalo ndilo litakolutumiwa na viongozi wote nchini toka ngazi ya chini hadi juu? Inawezekana au ndoto zangu tu?
Mnakumumbuka NYUMBU ya Mwalimu Nyerere. Je, kutokana na Internet inayoweza kukufundisha kutengeneza kila kitu huu kweli si ndio wakati wake. Au Watanzania tu bongolalal na wachovu kiasi hicho.
 
HIVI kuna wenzetu wanaamini kila kinachosemwa na Wafaransa au wazungu wengine. Nikupashe ndugu yangu Kagame hapendwi na Wafaransa kwa sababu ya chuki binafsi. Isitoshe kuanzia Januari 2009 Rwanda itakuwa nchi ya lugha tatu: Kiswahili, Kinyarwanda na Kiingereza. Kifaransa nje! Kwanini Wazungu wampende. Na angalia nchi yoyote ambayo kiongozi wake anapendwa na wazungu kwa kuwa 'ape' kila kitu hiyo lazima inakuwa nchi bomu tu, case in point, Ivory Coast, Egypt, Tunisia and so on!!
 

Nakubaliana na wewe. Nafikiri Wafaransa wanamchukia Kagame kwa vile anatakakubadili lugha ya taifa kutoka French kwenda kweny English. France is mad about it.

Kuhusu Genocide, wanataka kumzushia kuwa alimuua Byahalimana na kusababisha kuzuka kwa hiyo vurugu. Lakini ukifuatilia kwa karibu utagundua kuwa hiyo Genocide ilishapangwa hata kabla jamaa hawajafa, na akina Mseveni na Kagame walilishtukia hilo ndiyo sababu wakamuondoa. Imagine kama Habyalima angekuwa hai akaendesha hiyo genocide, sidhani kama watusi wangepona. Kufa kwake kulidistabilise everything na kufanya mambo yafanyike kienyeji. Ndipo Kagame akaweza kupata kuvu za kuwashinda kwa vile hawakuwa organised.

All in all tukubali Kagame ni makini kuliko JK wetu!!!!!!!!!!
 
wakisha uza alafu wawape wazee wa EAC nakuepuka laana alafu iweje...lol... watembelee magoti.. Radical thinking ridicules genuine concerns.. Hili ndio tatizo kubwa ya hizi forums.. A cyber mtikila of sorts..

Serikali iache tuu kununua magari yakifahari bila sababu yamsingi as a matter of policy at the highest levels, kama ni 10% I'm sure hakuna mtu ambae angekataa kati yenu simply because not taking it does not afford u anything in alternate... sana sana ukifa kama Omar Ali Juma watakucheka kwenu kuchafu thts all.. ndio watanzania tulivyo. Maamuzi yaukweli yafanyike at the highest level na yawe enforced tuu, wanunue magari 4wheel yanayoweza kufika sehemu nyingi zaidi tanzania na sio top of the range SUVs..

Kagame is by no means an exemplary leader..yani hii kweli ni forum.... in its truest etymological meaning.. Watu wanapayuka tuuu saa nyingine. Rather irritating for any1 with an actual brain.
 


Are you serious ndugu?
By the way siyo watanzania wote tuko hivo binafsi siko hivo kabisaaaa!

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, pamoja na kuwa Kagame si mwema sana lakini kwa kuwa strict na kuinua uchumi wa nchi yake he deserve it! Japo inanitia aibu sana kuona ka nchi kama kale kaliko gubikwa na vita uchumi wake unakua kwa kasi ya ajabu wakati TZ yetu iliyo jaa asali na maziwa umasikini unazidi kuongezeka kwa kiwango cha kutisha.
 

Vijiji vingine vinangefaidika zaidi kama hao viongozi wasingeenda, halafu vijiji vingepewa fedha ya mafuta amabyo yangetumiaka kuwapeleka huko (achilia mbali posho na marupurupu).
 

Wapande mabasi ya abiria kwa mikoa yote iliyo na barabara nzuri, hata hivyo kijijini kusiko barabara wapande punda. Pia treni au ndege (za abiria)kwa safari za mikoa ya mbali ni sawa.
Wenye ngazi ya kutumia SUV hamna anayelazimika kwenda kijiji mara kwa mara kama watawawezesha na kuwapa nguvu viongozi wa huko vijijini.
Ni wazi ni vigumu kwa CCM kuona gharama za SUV kwani toka lini CCM ikajua hali halisi ya TANZANIA? Waijuayo wao sio TANZANIA tunayoijua wengi na ndio maana wanaponda raha tu na SUV.
Kwa shughuli za hila siku, RAV au gari nyingine yeyote yenye injini 1.8-2LITRE, au yenye high chasis yeyote ingetosha tu kwenda kijijini.
Kwa kisingizio cha barabara mbaya, Nchi nyingi ulimwengu wa tatu km China, Bhutan, Mongolia nk zimewahi ingia kwenye mtego wa hizo gari kubwa (4000cc na zaidi) lakini wenzetu wakajua hali halisi mapema na bila kungojea kelele za raia serikali ikazipiga marufuku kwa matumizi ya kiserikali. Ni kitu cha kushangaza kuwa pamoja na aibu (?) ya misaada yote tuliyopokea mpaka hivi leo CCM haijarekebisha hilo. Kuna dalili kubwa kua wapinzani nao wataendekeza starehe za SUV endapo watachukua nchi, nawaombea watuletee mageuzi kwa hilo ama la sivyo na wao hawana mpango.
 
Hongera Mfumwa kwa kuleta hoja inayomgusa kila mtanzania wa kawaida, na kibaya zaidi ni jinsi hayo magari yanavyokuwa misused. Nilishuhudia mwenyewe kipindi hiki cha sikukuu ya christmas nikitoka Tanga kwenda Dar jinsi hayo magari yalivyobadilishwa na kuwa pickup za kubebea magunia ya mkaa, ndizi na mazao mengine, halafu mbaya zaidi gari linaonekana ni jipya lakini linatoa moshi sio kawaida.Nahisi hata hao ambao wako incharge na service za hayo magari wana namna wanafaidi katika fungu la maintenance.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…