Serikali yamzawadia Mbwana Samatta Kiwanja Maeneo ya Kigamboni!

Serikali yamzawadia Mbwana Samatta Kiwanja Maeneo ya Kigamboni!

Kiwe kiwanja cha kweli bhasi

Isiwe robo heka kama yangu nisiyejua hata danadana
 
Kama ni kweli wamefanya vzr italeta morali hata kwa wachezaji wengine kujituma wawapo kazini hili ndoto zao ziweze kutimia
Wangewapa viwanja wale waliowavunjia nyumba na hawana pa kulala now uyo anauwezo wa kununua kiwanja kwa sasa wangempa tu zawadi nyingine
 
WanaJF,

Serikali kupitia wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi imemzawadia Mbwama Samatta kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba 1200 (High Density) chenye thamani ya pesa za kitanzania milioni 20 maeneo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Zawadi hiyo imefuatia heshima kubwa ambayo kijana Mbwana Samatta ameipatia taifa kwa kushinda tuzo la mwana soka bora wa mwaka kwa wachezaji wa ndani ya Afrika.

Akizungumza na chanzo chetu cha habari waziri mwenye dhamana ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi ameeleza kuwa, kijana Samatta hakika anastaili kupata zawadi hiyo kutoka kwa serikali kwa heshima kubwa ambayo ameipatia Tanzania hususani kwenye soka la kimataifa.

Aidha, wadau mbalimbali wa soka wametoa hisia zao juu ya zawadi hiyo iliyotolewa na serikali kwa kijana Samatta kwa kusema kuwa, zawadi hiyo ya kiwanja inakuwa kama chachu kwa vijana wengine wa Kitanzania kujibidiisha zaidi katika sanaa na michezo kwa kuamini kuwa serikali ya awamu ya tano inathamini kazi zao.

kama 1200msq ni high density 400sqm itakuwa ni low density??????

ee mungu
 
Uko sawa ila kumbuka na muda hiyo bei ni wakati ule inauzwa kwa mara ya kwanza sasa muda umepita na thamani imeongezeka na watu wanavilipia kodi. Utakuwa unakumbuka vizuri ila umesahau na muda pia ni mali chukua hii

Nimekupata ! Nilikuwa na chemsha jukwaa na nikilenga jambo jingine.

Sawa natupa Jiwe Lumumba! Kwa bei hiyo Bomoa Bomoa itakuwa na mwisho kweli. Maana kiwanja tu 20.000.000 bei ya Serikali walalahoi wa kudunduliza Tofali hamsini hamsini ndoto ya Kiwanja kilichopimwa si ndiyo imekwisha mpita siku nyingi!

Waziri Lukuvi namshauri Serikali isifanye biashara badala yake ipime maeneo na kuwauzia kwa Bei ile ile ya mita moja kwa 3000 /Bei yakuwahamisha wenyeji wa Eneo husika na gharama zingine zitokane na Kodi zinazolipwa na Kila Mtanzania.

Mfano. Wakaazi wengi wa Maeneo ambayo Serikali/Halmashauri imepima Viwanja imewahamisha /kuwafidia wastani wa sh3000 kwa kila Mita ya Mraba- sasa kuiuza kwa 8000 na juu yake siyo haki hata kidogo na huku nikurudisha walalahoi nyuma.

WanaJF,

Serikali kupitia wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi imemzawadia Mbwama Samatta kiwanja chenye ukubwa wa mita za mraba 1200 (High Density) chenye thamani ya pesa za kitanzania milioni 20 maeneo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Zawadi hiyo imefuatia heshima kubwa ambayo kijana Mbwana Samatta ameipatia taifa kwa kushinda tuzo la mwana soka bora wa mwaka kwa wachezaji wa ndani ya Afrika.

Akizungumza na chanzo chetu cha habari waziri mwenye dhamana ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi ameeleza kuwa, kijana Samatta hakika anastaili kupata zawadi hiyo kutoka kwa serikali kwa heshima kubwa ambayo ameipatia Tanzania hususani kwenye soka la kimataifa.

Aidha, wadau mbalimbali wa soka wametoa hisia zao juu ya zawadi hiyo iliyotolewa na serikali kwa kijana Samatta kwa kusema kuwa, zawadi hiyo ya kiwanja inakuwa kama chachu kwa vijana wengine wa Kitanzania kujibidiisha zaidi katika sanaa na michezo kwa kuamini kuwa serikali ya awamu ya tano inathamini kazi zao.
hivi serikali Kwanini isituuzie sisi viwanja maana tunatapeliwa viwanja vya mabondeni
 
Serikali inapaswa kufanya zaidi ya hapa.. Kufanya kitu ambacho kitakuwa ni alama ya kitaifa kwa mfano kutangaza kujenga uwanja wa michezo hata mdogo tu kwa jina lake ili iwe kumbukumbu kwa vizazi vijavyo na huo Mchakato uanze kabla mambo hayajapoa ili wananchi na Wadau watoe support
 
kama 1200msq ni high density 400sqm itakuwa ni low density??????
wana jf naombeni msaada kati ya high density na low density ktk viwanja
 
Wewe wasema hayo, lakini Mbwana Samatta ame-dedicate tuzo yake kwa rais mstaafu Jakaya Kikwete. Kwa maana kuwa anatambua mchango wa rais katika mafanikio yake kisoka. Majungu sio mtaji. Jifunze kukubali tu.
yeye nae msenge tu aache kudedicate kwa babake anadedicate kwa wapita njia.asingezaliwa saa ngapi angeonwa na huyo muuza sura.
 
Good ...! Not better...!Best was need from the Government for Samata.
 
Yaani kiwanja kidogo sana hicho...

40 meters * 30 meters = 1,200...

Atleast wangempa cha 50m * 50m

Anyway zawadi ndogo sana kutokana na SIFA ALIYOIPATIA TZ...
Ila ingekuwa na umiss, demu ana makalio hapo, ungeona mamilioni na ekari moja anapewa... na gari juu... shit..!!
 
Vipi kuna ten percent au macho yangu?
Hivi viwanja si bei ya juu kwa kila mita za mraba silikuwa 10.000tsh ? Wadau mtanisaidia kama sikumbuki vizuri!
Kwa maana hiyo ingekuwa dhamani ya 1200x10000= 12.000.000tsh
Mkuu unaifahamu Kigamboni vyema? Hiyo mbona bei ndogo sana? Kuna maeneo ambayo bei zake ni mpaka 70,000 kwa square meter na hata zaidi.
 
Thamani ya juu kwa mita mraba moja iwe Tshs 10,000 kwani umesikia Kigamboni ni Mbinga?

Thamani ya juu inafika mpaka Tshs 20,000 kwa mita mraba moja siku hizi. Na kwa yale maeneo ya ufukweni inafika hadi Tshs 25,000 kwa mita mraba moja.
Mkuu, ufukweni inarange kati ya laki moja na nusu hadi laki 5 kwa square meter kutegemeana na location Kigamboni.
 
Mkuu unaifahamu Kigamboni vyema? Hiyo mbona bei ndogo sana? Kuna maeneo ambayo bei zake ni mpaka 70,000 kwa square meter na hata zaidi.

Nazungumzi Serikali kuuza kwa Bei hiyo iwe Kigamboni,mwanza au Mbeya-maana nilitegemea kuwa ingewawezesha walalahoi kupata Mahala pakujisitiri . Kwa Biashara kama Biashara hiyo Bei sishangai hata kidogo!
 
Back
Top Bottom