Serikali yangu Pendwa, Tumewakosea Nini Wafanya Biashara?

lolipo

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Posts
739
Reaction score
912
Kwa masikitiko makubwa sana ndugu zangu ninaleta malalamiko yangu kwa serikali yangu Pendwa, Hivi mnatutaka nini wafanya Biashara? Hizi restriction Mlizoweka kila mahali kuwa na uhitaji wa Kitmbulisho cha taifa, yani huwezi fanya kitu, halafu kitambulisho mnatoa nyie, huu ni mwaka sasa HAKUNA kitambulisho, maana yake ni nini Jamani?

Nikaambiwa niende brela pale basi kuna namna naweza kipata, nimetoka mkoani mpaka dar, nimekaa week 1 nimetumia zaidi ya laki 5, na sijakipata, sasa mimi nina swali, nina uhakika kuna watu kama mimi kwa mamilioni ambao hata mngesema kitambulisho ni laki 3 ningelipa, maana nishapoteza laki 5 tayari, na sijakipata!

SWALI KWA SERIKALI YANGU PENDWA, MBONA KAMA MNAKOMOA SASA?
 
Duuh mimi nimehangaika mno na bado sijakipata soon nitaweka namba ya kigogo mmoja hapa (kangi lugola ) kila mtu amtumie sms ya kudai kitambulisho labda tutapatiwa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sidhani kama comment yangu itakua msaada sana but what I want to tell you and other entrepreneurs is this, wakati mwingine mtakapokua mnapiga kura chagueni viongozi watakao jali maslahi ya biashara zenu and not other wise!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Watanzania ndio wanachagua rais, sio wafanya biashara
 
NIDA kuna rushwa
 
Hii nchi ili uwe na amani labda uwe umekaa tu.

Ukijaribu kujishughulisha kwa namna yoyote tu, lazima utakwama kutokana na kuwa na watawala wasio na dira na wanaotumia tabia zao binafsi kuendesha nchi.
Watu wanajitolea kupigania taifa lao mambo yabadiliK
 

Kama hiki kitambulisho ni changamoto, si waweke gharama, kwa sasa mimi hat wakinambia laki 5 nitatoa tu haina shida, wamebana kote kote, nafanyaje sasa?
 
NIDA kuna rushwa

Ila kwa nini wasifanye official vinalipiwa tulipe tuendelee, aliyeweka masharti ni serikali, ambaye anawajibika kutoa vitambulisho ni serikali, tunafanyaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…