Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,172
Pinda katangaza hivi punde mjini Dodoma kuwa baada ya kelele nyingi za wananchi, viongozi wa dini na wabunge, serikali imeamua kugeuza uamuzi wake wa kufuta misamaha ya kodi kwa taasisi za dini. Amesema Mkulo atatangaza kesho jinsi serikali itakavyopfidia pengo la fedha linalotokana na uamuzi huo
Hiyo ni weakness kubwa sana, mpaka sasa sijaona sababu kwa nini wasitozwe kodi kwenye non-spiritial services.
Nitawaunga mkono tu kama watapunguza matumizi ya serikali, kutangaza kuuza VX zote... na waziri apewe SUV [RAV 4, Honda, Suzuki Vitara]!!!
MN,
Kwa hiyo hiyo misamaha ilikuwa sahihi kabisa kuiondoa though kuna ukweli kwamba kuna baadhi ya taasisi ambazo zinaitumia misamaha hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa!
Next Level,
Hata ikiwa wanatumia vizuri, lakini wajameni taasisi za dini kazi yao ni kueneza neno la Mungu!
Kazi zao sio ku-run government parallel to government ya kaisari, haya mambo ya shule na hospital za taasisi za dini in reality ni services za kutolewa na serikali ikiruhusiwa kupokea kodi.
Uamuzi mzuri sana huu maana mantiki ya misamaha hii ililenga zaidi kuudidimiza ukristo. Angalia mifano aliyoitoa Mkulo inahusu Makanisa tu. Pia hakukuwa na mantiki kuwaadhibu Wakristo wote kwa makosa ya wachache. Sheria ziko wazi. Atakayekiuka ndiye aadhibiwe. Kwa mfano dhehebu au shirika la dini lilitakiwa liagize magari kwa ajili ya shughuli za kiroho halafu lenyewe likayaingiza kwa ajili ya biashara. Kinachofuata ni kulichukulia hatua shirika au dhehebu husika. Sio kuyachukulia na madhehebu mengine ambayo hayajakiuka taratibu na kuyafutia misamaha kwa kosa la wachache! Ile kauli ya Mkulo kwamba "uamuzi huu wa kufuta baadhi ya misamaha haukufanywa kwa sababu yeye na Rais Kikwete ni waislamu bali uamuzi ulifanywa wakati wakristo ni wengi waliohusika na uamuzi huo". Hivi hapa anataka kueleza nini? Wakristo walio wengi wanaangalia kwa makini mwenendo wa Serikali hii ya Awamu ya Nne!

\MN,
Huu ni ubabaishaji wa hali ya juu kwa serikali yetu.....inamaana hawakufanya utafiti wa kutosha kabla ya kufanya maamuzi ya awali ndugu zangu?
To me it was very right decision ya kuondoa ile misamaha ya kodi hasa ukizingatia these days the so called churches and other religious organs are mushrooming only to claim the benefits of tax exemptions granted to them for their personal benefits!
Kwa hiyo hiyo misamaha ilikuwa sahihi kabisa kuiondoa though kuna ukweli kwamba kuna baadhi ya taasisi ambazo zinaitumia misamaha hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa!
\
NextLevel
Ulisikiliza alichokisema leo Bungeni Mheshimiwa Lucy Mayenga, Viti Maalum (CCM)? Amesema watendaji wengi serikalini ni wazembe, wasio na ubunifu, wasiojua kazi na wenye kujawa na ubinafsi kiasi kwamba utendaji wao umekuwa kero. Amesema Serikali haipaswi kuwavumilia watu kama hawa ambao kila mwaka "wanashughulikia" kupata ufumbuzi wa matatizo yale yale! Amesema sasa umefika wakati wa kuwaondoa watu hao, wasivumiliwe kwa kuwa wamekuwa na utendaji wa muda mrefu serikalini! They have to go! Yaani, sasa, Serikali inapaswa kuendeshwa kama PRIVATE SECTOR, kwani, hata mimi ninamuunga mkono Mhe. Mayenga! Nani aliyesema kwamba Serikalini ndio kimbilio la wazembe wote waliofukuzwa kazi kwenye PRIVATE SECTOR?
Kukujibu swali lako hapo juu, NDIO, hakuna utafiti wa kina uliofanywa kabla ya Serikali kufikia uamuzi wa kufuta misamaha ya kodi kwa NGOs na Taasisi za Kidini! Hakuna!
Wamesema kwamba wamegundua matukio ya wizi, yaani, watu walioingiza vitu kadhaa kwa "gia" ya NGO na Taasisi za Kidini, lakini vitu hivyo vikaishia mitaani, kwenye maduka, kama bidhaa za kawaida. Sukari, nguo, mabati, na kadhalika!
Sasa, kama alivyosema Dr. Slaa (nadhani leo Bungeni), kwa nini basi Serikali isiwakamate na kuwashughulikia hao Makasisi, Mapadre, Maimamu na Masheikh waliolihujumu taifa letu? Si kuna ushahidi? Huo ni uhalifu tu kama ulivyo uhalifu mwingine.
Serikali "haikunywea", kumekuwa na UZEMBE ulioanzia kwa Mshauri Mkuu wa Waziri wa Uchumi katika suala hili, yaani, Mama Mary Nagu, ambako muswada huo wa kuondoa misamaha ya kodi ulikotokea, Mkullo yeye akaingia KICHWA KICHWA, fumba na kufumbua, bila hata a DUE DILLIGENCE (hivi hiki kitu kitazungumziwa mpaka lini?), wameleta muswada bungeni usio na kichwa, utumbo wala miguu! Kha!
./Mwana wa Haki
Mwanahaki you said it all nimeandika kuonyesha msisitizo tu....but I conquer with you comments 100%
Cheers
Inavyoelekea serikali haikupima upepa maana hii ni kigeugeu kweli. lakini nadhani pia wameangfalia na Oktoba 2010 na hii elimu ya uraia inayotolewa na wakatoliki, iwapo wataamua kuunganisha na kampeni zao, hali inaweza kuwa mbaya kwa muungwana mwakaniMN,
Huu ni ubabaishaji wa hali ya juu kwa serikali yetu.....inamaana hawakufanya utafiti wa kutosha kabla ya kufanya maamuzi ya awali ndugu zangu?
To me it was very right decision ya kuondoa ile misamaha ya kodi hasa ukizingatia these days the so called churches and other religious organs are mushrooming only to claim the benefits of tax exemptions granted to them for their personal benefits!
Kwa hiyo hiyo misamaha ilikuwa sahihi kabisa kuiondoa though kuna ukweli kwamba kuna baadhi ya taasisi ambazo zinaitumia misamaha hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa!
Kaka kama unafikiria hivyo then una tatizo! Ila in any case huu ni uamuzi uliofanyika kwa sababu mwaka unakuja ni uchaguzi, imesogezwa mbele tu... serikali yoyote huko mbele especially angalia budget ya 2011/12... hiyo misamaha itakuwa imeondolewa.
Kwa kweli msimamo wangu unabaki kuwa dini ni kitu personal ambacho hakiwahusu watu wengine ambao si members wa dini hiyo. Kuendelea kutoa misamaha ya kodi kwa dini ni kutoa preference kwa wenye dini. Wasio na dini nao wanavyo vitu personal wanavyovipenda lakini havisamehewi kodi. Dini ni personal sawa na unywaji wa pombe au uvutaji wa sigara. Wenye dini wanastahili kulipia vifaa vyao vya ibada kama wanavyolipa sadaka na zaka makanisani bila kuhoji matumizi yake.
Hata hivyo, logic ya kumsamehe kodi Barick gold na kumtoza kodi mwenye kanisa ndo inayofanya ni withdral support yangu kwa suala hilo.
Mikataba ya madini iliyosainiwa iko juu ya sheria zote zitakazotungwa mpaka muda wa mikataba ile utakapoisha. Nilishangaa nilipogundua kuwa misamaha iliyofutwa kwenye madini ni kwa makampuni ambayo hayajaingia nchini yaani makampuni ambayo hayapo. Yale yaliyopo misamaha kama kawaida.
Sasa ikiwa hawa wanaozalisha faida kubwa huko kwao wanaachiwa halafu tunatozana sisi hata kwenye vifaa vya ibada, huu ungekuwa utaahira. Kwanza kodi yenyewe ingekuwa only symbolic.
Kwa hiyo aliyeileta kodi hiyo aliazimia kuzikomoa taasisi za kidini ambazo anadhani hazimhusu.