\
NextLevel
Ulisikiliza alichokisema leo Bungeni Mheshimiwa Lucy Mayenga, Viti Maalum (CCM)? Amesema watendaji wengi serikalini ni wazembe, wasio na ubunifu, wasiojua kazi na wenye kujawa na ubinafsi kiasi kwamba utendaji wao umekuwa kero. Amesema Serikali haipaswi kuwavumilia watu kama hawa ambao kila mwaka "wanashughulikia" kupata ufumbuzi wa matatizo yale yale! Amesema sasa umefika wakati wa kuwaondoa watu hao, wasivumiliwe kwa kuwa wamekuwa na utendaji wa muda mrefu serikalini! They have to go! Yaani, sasa, Serikali inapaswa kuendeshwa kama PRIVATE SECTOR, kwani, hata mimi ninamuunga mkono Mhe. Mayenga! Nani aliyesema kwamba Serikalini ndio kimbilio la wazembe wote waliofukuzwa kazi kwenye PRIVATE SECTOR?
Kukujibu swali lako hapo juu, NDIO, hakuna utafiti wa kina uliofanywa kabla ya Serikali kufikia uamuzi wa kufuta misamaha ya kodi kwa NGOs na Taasisi za Kidini! Hakuna!
Wamesema kwamba wamegundua matukio ya wizi, yaani, watu walioingiza vitu kadhaa kwa "gia" ya NGO na Taasisi za Kidini, lakini vitu hivyo vikaishia mitaani, kwenye maduka, kama bidhaa za kawaida. Sukari, nguo, mabati, na kadhalika!
Sasa, kama alivyosema Dr. Slaa (nadhani leo Bungeni), kwa nini basi Serikali isiwakamate na kuwashughulikia hao Makasisi, Mapadre, Maimamu na Masheikh waliolihujumu taifa letu? Si kuna ushahidi? Huo ni uhalifu tu kama ulivyo uhalifu mwingine.
Serikali "haikunywea", kumekuwa na UZEMBE ulioanzia kwa Mshauri Mkuu wa Waziri wa Uchumi katika suala hili, yaani, Mama Mary Nagu, ambako muswada huo wa kuondoa misamaha ya kodi ulikotokea, Mkullo yeye akaingia KICHWA KICHWA, fumba na kufumbua, bila hata a DUE DILLIGENCE (hivi hiki kitu kitazungumziwa mpaka lini?), wameleta muswada bungeni usio na kichwa, utumbo wala miguu! Kha!
./Mwana wa Haki