Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,172
- Thread starter
-
- #21
Na nini kimetokea ghafla hadi kugeuza sababu hizo na kuifanya serikali kubatilisha uamuzi wake?Unajua kinachogomba hapa ni sababu ya kufuta hiyo misamaha...
Ni kweli kuwa dini ni kitu personal. Ila kinapokuwa haki-generate profit sioni sababu ya kukitoza ushuru. Vile vile taasisi za dini zina mchango mkubwa kwa amani na utulivu wa jamii yetu. Mafundisho yanayotolewa na dini mbalimbali huisaidia sana serikali kupata nafasi ya kuongoza. Kwa maana nyingine, dini ni silaha mojawapo ya serikali. Hili pia linajitokeza katika ushiriki wa dini mbalimbali katika utoaji wa huduma za jamii kama mashule, hospitali n.k.Kwa kweli msimamo wangu unabaki kuwa dini ni kitu personal ambacho hakiwahusu watu wengine ambao si members wa dini hiyo. Kuendelea kutoa misamaha ya kodi kwa dini ni kutoa preference kwa wenye dini. Wasio na dini nao wanavyo vitu personal wanavyovipenda lakini havisamehewi kodi. Dini ni personal sawa na unywaji wa pombe au uvutaji wa sigara. Wenye dini wanastahili kulipia vifaa vyao vya ibada kama wanavyolipa sadaka na zaka makanisani bila kuhoji matumizi yake.
Kama hii ni kweli, basi ni dalili ya serikali kutokuwa makini. Maana ni kwamba, kuna sheria kwa makampuni yasiyokuwepo na yale yaliyopo. Ni kweli hii?Hata hivyo, logic ya kumsamehe kodi Barick gold na kumtoza kodi mwenye kanisa ndo inayofanya ni withdral support yangu kwa suala hilo.
Mikataba ya madini iliyosainiwa iko juu ya sheria zote zitakazotungwa mpaka muda wa mikataba ile utakapoisha. Nilishangaa nilipogundua kuwa misamaha iliyofutwa kwenye madini ni kwa makampuni ambayo hayajaingia nchini yaani makampuni ambayo hayapo. Yale yaliyopo misamaha kama kawaida.
Nina uhakika kuwa kesho Mkullo atakapotangaza mabadiliko ya Bajeti yake, atarudisha misamaha/mapunguzo ya kodi yaliyotolewa na serikali kwenye ile ya kwanza. Mapunguzo ya VAT hadi 18% sasa yatarudi kama yalivyokuwa. Sina uhakika kama anaweza kurudisha ushuru wa meli ambao ulikuwa umefutwa hapo awali.Sasa ikiwa hawa wanaozalisha faida kubwa huko kwao wanaachiwa halafu tunatozana sisi hata kwenye vifaa vya ibada, huu ungekuwa utaahira. Kwanza kodi yenyewe ingekuwa only symbolic.
Kwa hiyo aliyeileta kodi hiyo aliazimia kuzikomoa taasisi za kidini ambazo anadhani hazimhusu.
Clever men know how to solve their problems, but wise ones know how to avoid them
Hiyo ni weakness kubwa sana, mpaka sasa sijaona sababu kwa nini wasitozwe kodi kwenye non-spiritial services.
Nitawaunga mkono tu kama watapunguza matumizi ya serikali, kutangaza kuuza VX zote... na waziri apewe SUV [RAV 4, Honda, Suzuki Vitara]!!!
Uamuzi mzuri sana huu maana mantiki ya misamaha hii ililenga zaidi kuudidimiza ukristo. Angalia mifano aliyoitoa Mkulo inahusu Makanisa tu. Pia hakukuwa na mantiki kuwaadhibu Wakristo wote kwa makosa ya wachache. Sheria ziko wazi. Atakayekiuka ndiye aadhibiwe. Kwa mfano dhehebu au shirika la dini lilitakiwa liagize magari kwa ajili ya shughuli za kiroho halafu lenyewe likayaingiza kwa ajili ya biashara. Kinachofuata ni kulichukulia hatua shirika au dhehebu husika. Sio kuyachukulia na madhehebu mengine ambayo hayajakiuka taratibu na kuyafutia misamaha kwa kosa la wachache! Ile kauli ya Mkulo kwamba "uamuzi huu wa kufuta baadhi ya misamaha haukufanywa kwa sababu yeye na Rais Kikwete ni waislamu bali uamuzi ulifanywa wakati wakristo ni wengi waliohusika na uamuzi huo". Hivi hapa anataka kueleza nini? Wakristo walio wengi wanaangalia kwa makini mwenendo wa Serikali hii ya Awamu ya Nne!
Hivi watu wengine msipoandika pumba huwa hamjisikii raha??
Serikali kama itabadilisha uamuzi huo itakuwa imechemsha sana, hii misamaha ya kodi ndio chanzo kikubwa cha rushwa.
Next Level,
Hata ikiwa wanatumia vizuri, lakini wajameni taasisi za dini kazi yao ni kueneza neno la Mungu!
Unaweza kusimama mahali na ukahubiri neno la Mungu wakati wahumini wanaumwa na hawana huduma ya matibabu, hata kama ipo hawawezi kuchangia au zipo mbali. Viongozi wa dini wanaelekezwa kuponyesha wahuni kiroho na kimwli, ndiyo maana miskiti inachimba visima, shule nk.. ili wahumini wao wasipate shida mahali walipo.
Hata wamisionari walipokuja walijenga makanisa, shule, hospitali nk.
Kazi zao sio ku-run government parallel to government ya kaisari, haya mambo ya shule na hospital za taasisi za dini in reality ni services za kutolewa na serikali ikiruhusiwa kupokea kodi.